MwanaKijiji.COM

Wednesday
Feb 08th
Text size
  • Increase font size
  • Default font size
  • Decrease font size
Home arrow Business arrow Biashara arrow Dowans na deni la Dola Mil. 75!
Dowans na deni la Dola Mil. 75!
(1 vote)
Written by Kulikoni   
Thursday, 12 March 2009
Exclusive WAKATI sakata la ununuzi wa mitambo ya kuzalisha umeme inayomilikiwa na kampuni ya Dowans Tanzania Limited likiendelea kupamba moto, uchunguzi wa KULIKONI umebaini kuwa Serikali ya Tanzania iwapo ingeng’ang’ania kuinunua, ingeingia hasara ya karne kwani mitambo hiyo ina deni kubwa benki linalofikia dola za Marekani milioni 75 (zaidi ya bilioni 100/-).
Uchunguzi huo wa kina umebaini kwamba kati ya Aprili 30 na Novemba 9, 2007, ikiwa ni miezi kadhaa baada ya kuhaulishiwa mkataba kutoka Richmond, Dowans Tanzania Limited ilikopa fedha katika benki mbili tofauti za Barclays na Stanbic zinazofikia bilioni 97.5/- na kuiweka dhamana mitambo hiyo ya kuzalishia umeme iliyoko Ubungo na mali zote za kampuni hiyo walizonazo sasa na zote ambazo zitapatikana baadaye.

Mitambo hiyo ambayo hadi sasa ipo katika viwanja vya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) ndiyo ambayo kampuni hiyo sasa imetangaza kuiuza na mteja mkubwa alionekana kuwa ni Serikali ya Tanzania ambayo ilielezwa kuwa na nia hiyo kabla hata ya mitambo hiyo kuanza kazi.

Nyaraka ambazo KULIKONI linazo, zinaonesha kuwa Dowans walikopa jumla ya dola za Marekani milioni 55 kutoka Barclays na dola nyingine milioni 20 za Marekani kutoka Stanbic tawi la Tanzania, fedha ambazo zinapaswa kulipwa kwa riba na gharama nyinginezo.

Dowans walipokopa dola za Marekani milioni 20 kutoka Stanbic tawi la Tanzania, dhamana iliyotajwa ni mitambo ya kuzalisha umeme, akaunti yao, mikataba, bima, na amana zote za kampuni hiyo tata.

Katika mawasiliano na kampuni hiyo benki ya Stanbic yenye makao yake makutano ya Barabara ya Ali Hassan Mwinyi na Kinondoni, Dar es Salaam, iliwakilishwa na Helen Makanza na Jeff Daly wakati Dowans haionyeshi ni nani aliyewakilisha kampuni hiyo zaidi ya Wakili Samson Russumo, ambaye alikuwa Kamishna wa Kiapo.

Baadaye Juni, 2007, Dowans ilichukua mkopo mwingine wa dola za Marekani milioni 20 kutoka benki ya Barclays ya Mauritius, makubaliano yaliyoelezwa kufuata sheria za Uingereza.

Miezi minne baadaye, Dowans imebainika walichukua tena kiasi cha dola za Marekani milioni tano kutoka Barclays tawi la Tanzania, dhamana ikiwa ni mali zile zile zilizotumika kuchukua mkopo kutoka Stanbic na Barclays ya Mauritius.

Kampuni hiyo ambayo hadi sasa wamiliki wake upande wa Tanzania hawajulikani dhahiri, inaonekana katika nyaraka nyingine kuweka rehani mali zake na kuchukua dola za Marekani milioni 30, Novemba 9, 2007.

Tayari Tanesco kupitia Mkurugenzi wake Mtendaji, Dk. Idris Rashidi, imekwishajitoa kununua mitambo hiyo ya Dowans ‘kwa shingo upande’ huku ikiwatisha Watanzania kwamba watapata matatizo makubwa ya umeme kwa “kutofanya uamuzi sahihi,” huku wito wa kutaka wahusika wote walioingiza nchi katika matatizo wajiuzulu na kuchukuliwa hatua ukiendelea.

Kabla ya Tanesco kujitoa kununua mitambo hiyo, wadau mbalimbali akiwamo Spika wa Bunge, Samuel Sitta, waliitahadharisha serikali kuhusu mpango wake wa kununua mitambo ya Dowans.

Sitta aliishauri serikali kufuata ushauri wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini ambayo ilipendekeza kwa serikali kuachana na mchakato wa kununua mitambo hiyo.

Tanesco walitaka kununua mitambo hiyo kutoka Dowans kwa dola za Marekani milioni 69 sawa na bilioni 90/-, kiwango ambacho kimeelezwa kwamba ni kikubwa mno na huenda kililenga kulipia deni la benki ambalo kampuni hiyo inadaiwa hadi sasa.

Tayari Dowans wamefungua mashtaka kwenye Baraza la Kimataifa la Usuluhishi Paris, Ufaransa huku Tanesco wakiwa wamefungua kesi Tanzania wakitaka mali za Dowans zizuiwe hadi hapo shauri la Ufaransa litakapokwisha.

Awali, Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja naye alikaririwa akisema kwamba serikali inaunga mkono ununuzi wa mitambo hiyo ya Dowans kutokana na hali halisi ya nishati nchini na kwamba uamuzi huo ndio sahihi kwa wakati huu na hauhusiani na ufisadi wowote, kauli iliyopingwa na wadau wengi.

Miongoni mwao ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini, William Shellukindo na makamu wake, Dk. Harrison Mwakyembe, ambao wote walisisitiza kwamba ukosefu wa umeme utatokana na uzembe wa uongozi wa Tanesco na si kwa kutonunuliwa mitambo ya Dowans na kwamba upo uwezekano wa kupata mitambo mipya kwa bei mwafaka.

Nyaraka zinaonyesha kwamba Kampuni ya Dowans (T) Ltd, inamilikiwa kwa asilimia 61 na kampuni ya Dowans ambayo inatajwa kuwa na makao yake nchini Costa Rica, na asilimia 39 na kampuni ya Portek, yenye makao yake makuu Singapore.

Dowans inatajwa kuhusishwa na raia wa Oman mzaliwa wa Zanzibar, Suleiman Mohamed Yahya Al Adawi, ambaye hata hivyo uhusiano yake na wanasiasa wa Tanzania unatia shaka.

Utata wa Richmond uliwaponza aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa na mawaziri wawili waliowahi kuongoza Wizara ya Nishati na Madini, Nazir Karamagi na Dk. Ibrahim Msabaha, ambao walilazimika kujiuzulu ndani ya Bunge kwa kuhusishwa kwao na kashfa ya mradi huo wa umeme wa dharura.

Hata hivyo pamoja na kuushindwa mradi huo na kuhaulisha kazi zake kwa Dowans Richmond imekuwa ikijinasibu katika tovuti yake kwa kuanzisha mradi huo na kufanya maandalizi ya sehemu kubwa ya kukamilishwa kwa mradi huo.

Maswali:
Kwanini walikuwa wanashinikiza tununue mitambo hii ya Dowans? Je inajalisha kama mitambo imewekwa rehani kwenye deni/madeni ya kibenki? Je wale waliokuwa wanataka serikali (walipo kodi wa Tanzania) wanunue majenereta haya walikuwa wanajua juu ya deni hilo?
Comments (7)add comment
mkamaimba: ...
Waliokuwa wakishabikia Serikali inunue mitambo hiyo Dr. Rashid na Bill Ngeleja wote wakiwa waajiriwa zamani wa ROSTAM AZIZ huko (ACB na Vodacom) Wanafahamu fika hilo kwamba mitambo kwani inaeleweka kwamba ACB ilikuwa kama Referee wa DOWANS ndiyo maana akina Msabaha wakalazimisha Idris apewe madaraka ya kuwa CEO wa TANESCO na malengo ni kufanikisha maslahi ya mafisadi kwenye taasisi hiyo ikiwepo kuunganisha kiutapeli umeme kule BUZWAGI, kuhakikisha msamaha wa Kodi kwa AGGREKO umeheshimiwa,mitambo ya DOWANS imenunuliwa NA KUHAKIKISHA kwamba tanesco wananunua kwa kiasi cha ASILIMIA 100 umeme kutoka SONGAS ili walipwe CAPACITY charge yote huku mtambo mpya uliozinduliwa na JK usitumike eti gesi ni aghali. Ndio maana Bill alipata ujasiri wa kumtetea Idris kuhusu nchi kuingia GIZA na huku Jakaya Kikwete amaekaa kimya yeye ni SWAHIBA MKUBWA wa ROSTAM na kamwe hayuko tayari kuvunja ndoa yao na Hakuna mtu yeyote kwenye Serikali au CCM mwenye ubavu wa kuyasema hayo hadharani. AKASULIZWE Jakaya Kikwete NI kwa vipi ameteua mtu mgonjwa kuwa Mwenyekiti wa BODI Peter Ngumbulu imefanyika maksudi ili Dr. Idris awe huru kufanya ubabe. Kwanza ni mstaafu he is above Sixty YEARS old Mbona wengine wanapaswa kustaafu. Huu si uvunjwaji bayana wa sheria za nchi? Kwanza anapewa mshahara millioni ishirini kwa mwezi.(20,000,000/) HUU NI UFISADI SQUARED AIBU KWA SERIKALI YA CCM KUNA SIKU UMMA UTAFUKUA HATA MAKABURI YENU ILI KUEWAHOJI!
1

March 16, 2009
Votes: +0
ando kinana: ...
Kama Dowans wana deni kama hili na bado hatuwataji then ule mkwaruzo aliopata CCM unaanza kuwa donda ndugu

Miezi minne baadaye, Dowans imebainika walichukua tena kiasi cha dola za Marekani milioni tano kutoka Barclays tawi la Tanzania, dhamana ikiwa ni mali zile zile zilizotumika kuchukua mkopo wa dola milion 20 kutoka Stanbic na Barclays ya Mauritius.
2

March 19, 2009
Votes: +0
mugerezi: ...
mhh kwakweli hii nayo ni kali maana bila ya habari kama hizi unaweza kupingwa changa la macho. Tatizo la serikali yetu wao wanalazimisha kuwa kuna maslahi fulani hapo otherwise hata kuongelea tu ilitakiwa jamaa hawa wapelekwe mahakamani kwa kujaribu kuiibia serikali kwa kuizua mitambo ambayo haipo.
3

March 20, 2009
Votes: +0
RITCHIEB: ...
Mungu ibariki Tanzania na walalahoi wote ! kwani tunaishi mradi tuishi, eeh mungu tunaomba siku moja mfufue baba wa taifa angalau kwa siku moja tu ayaone haya kwa vijana wake aliowategemea leo hii wanavyo mgeuka , just imagine retired man anaitwa special kupewa madaraka ya kuididimiza nchi Dr Idrisa na usomi wako kuwa mshahara millioni ishirini kwa mwezi.(20,000,000/) ni halali ? ina maana Tanzania hatuna talented vijana waliosoma na wenye upeo wa kisasa kuliko huyo mzee kipara kweli , mbona vijana tumesoma wengi wana MAPHD lakini hawapewi nafasi ya kuonyesha elimu yao JK unawabana sana . Nakuhakikishia Mwanakijiji kuna vijana waliosoma na wenye upeo mkubwa kuliko hawa wazee na wana uwezo wa kuibadilisha nchi na kuleta maendeleo makubwa na ya kisasa pasipo kubagua nani wala nani , hii ndio inayosababisha vijana wengi kuikimbia nchi ukionekana una uwezo kidogo kushinda watoto wao basi utafanyiwa fitina au hata kuawa ndio maana vijana wengi wanaishia EXIL , Mfano mzuri DR LIPUMBA kwetu tunamzarau amekwenda kufanya makubwa sana serikali ya uganda, ona mseveni anavyojidai sasa eeeh mungu lini wazee hawa wataacha kutuloga sisi vijana kwanza muda wao umeshakwisha watoke madarakani nchi inajengwa na vijana sio wazee mnataka hadi mfie madarakani jamani ?
MBONA MWANAKIJIJI NILISIKIA UWAKALA WA RICHMOND LOWASA ALIMSHIRIKISHA MWANAE FREDDY LOWASSA , WAKATI KAMPUNI HIYO HIYO YA KINA FREDDY LOWASSA INA WAKURUGENGI WAWILI RIDHIWANI KIKWETE NA FREDDY LOWASSA iko opposite ATC House mbona hili kimya au sababu limemshirikisha mtoto wa kikwete ? tupieni macho hapo jamani
4

March 21, 2009
Votes: +0
Mwana: ...
smilies/angry.gif jamani mbona watanzania mnatia aibu, yaani kila siku ni malumbano ya viongozi tu mtaelimika lini ndio maana watu wakishakuja nchi za watu huku wanaogopa kurudi nyumbani maana kila siku unachosikia ni kumhusudu na kumuona mwenzie kapata , lakini yeye mwenyewe kujitahidi na kuhusudu ili awe kama alivo watoto wa kikwete na Lowassa na hatawa Hamad Rashid na Seif Shariff wanaendelea wote wanasoma nje na wakirudi nyumbani wanapata kazi nzuri na kuendelea husudu maendeleo sio maneno. Watoto wa viongozi wa upinzani wote wanasoma nje ya Tanania lakini nyinyi wananchi mnawasakama wa viongozi wa ccm iliochoka acheni ujinga endelezeni nchi mna kila kitu hata mbolea ya kuku ni mali wachilia mbali ilivo mbolea ya takataka. hakuna kisichokuwa mali Tanzania tuna bahati kubwa aliyotupa Mungu lakini penye miti hakuna wajenzi mnalala nje. Ngojeni wakenya na waganda watakavokuja kula na kutajirika na mali zetu Kikwete atakapomaliza kuuza nchi!
5

March 29, 2009
Votes: +0
Simo: ...
Mwana yawezekana umeridhika na kila kitu kinachoendelea ktk nchi hii. Ninyi ni kama watu ambao sikio la kufa halisikii dawa. Kimya kikiendelea hawa watu watatumaliza hebu angalia leo rasilimali ya nchi hii inavyoporwa halafu tuendelee kukaaa kimya. Kuna msemo huu you reap what you sow. Muda si muda hawa mafisadi watavuna walichopanda hebu kumbuka m,ambo ya Mobutu Seseko.
6

April 23, 2009
Votes: +0
Mbega Mzuri: ...
Nadhani haya ndiyo matunda halisi ya kuwaogopa wanaotumia fedha za bangi ambao mwalimu jkn aliwakataa. najiuliza, tunaelekea wapi sasa.
7

September 18, 2009
Votes: +0

Write comment

busy
 
Ni nani anafaa kuingoza Tanzania kama Rais kuanzia 2010-2015?
 

Photo Albums

Just $6.95/Mo
Unlimited Space, Unlimited Transfer, Free Domain
www.bluehost.com

MwanaKijiji.COM LIVE

Window Player   RealAudioPlayer   Itune Player