MwanaKijiji.COM

Wednesday
Feb 08th
Text size
  • Increase font size
  • Default font size
  • Decrease font size
Home arrow Business arrow Biashara arrow Dr. Idris Rashid: Kujiuzulu? Majenereta kutonunuliwa?
Dr. Idris Rashid: Kujiuzulu? Majenereta kutonunuliwa?
(0 votes)
Written by M. M. Mwanakijiji   
Thursday, 05 March 2009
ExclusiveKwa karibu masaa sita ka nzi kalikuwa kametulia kwenye ukumbi makao makuu ya Tanesco ambapo Mkurugenzi wa Shirika hilo Dr. Idris Rashid alikuwa aje kuzungumza na waandishi hususan suala kununua majenereta ya kufulia umeme ambayo yanamilikiwa na kampuni yenye utata wa umiliki wake na yenye kuhusishwa na kampuni ya kifisadi ya Richmond, Dowans. Hata hivyo, muda si mrefu uliopita mtumishi wa Tanesco aliingia ukumbini na kuwaambia waandishi waliokuwa wanasubiri kwa muda mrefu kuwa Bw. Idris hatozungumzia nao na kuwaomba radhi.

Hata hivyo, vyanzo vyetu vyenye uwezo wa kupenya kuta na madari vinadokeza kuwa suala la Dowans limefikia mahali pagumu ambapo sasa Tanesco wako tayari kuachana na wazo hili ili kutafuta vyanzo vingine vya umeme wa dharura na ya kuwa wametilia maanani "kelele" za wadau mbalimbali. Hili linakuja baada ya sauti za Spika wa Bunge la Muungano Mhe. Samuel Sitta na Mbunge wa Kyela Mhe. Harrison Mwakyembe kupaza sauti zao kupinga mpango huo. Ujumbe ambao umepokelewa toka kwa watunga sheria hao ni kuwa yeyote atakayenunua majenereta ya Dowans ajiandae kuwajibika Dodoma kama walivyowajibishwa wengine!

Tishio hilo ambalo limepokelewa kwa hisia ya kunyong'onyea limetuma ujumbe ulio wazi kuwa endapo serikali itatekeleza au kutoa baraka kwa Tanesco kufanya kitu ambacho wanajua hawapaswi kufanya basi patakuwa hapakaliki. Hadi hivi sasa kundi kubwa la wabunge waliosimama upande wa ripoti ya Kamati Teule kuhusu Richmond, limeshajipanga tayari kuanzisha "kasheshe" jingine ambalo linaweza kabisa kuitikisa serikali.

Hata hivyo, Dr. Idris inaonekana bado amekuwa na 'kichwa ngumu' hasa baada ya serikali na kamati za Bunge zote kuiachia uamuzi wa mwisho kuhusu suala la mitambo. Hata hivyo, kuna imani kuwa alichofanyiwa Dr. Idris ni kupewa kisu ashike, tatizo ni kuwa amepewa upande wa makali huku mpingi ukiwa umeshikwa na wengine ambao wako tayari kuuvuta.

Kutokana na hili, kuna kila dalili Dr. Idris anaweza kutangaza kujiuzulu wadhifa huo kitu ambacho alijaribu kukifanya muda si mrefu uliopita kuhusiana na suala la kampuni ya saruji ya huko Tanga. "Hayuko tayari kujitundika mwenyewe kitanzini kwa kamba yake mwenyewe!" amedokeza mmoja wa watu wanaojua suala hilo.

Sasa hivi kinachosubiriwa ni muda tu kuona Dr. Idris atafanya nini huku akijua kuwa tayari anahusishwa na kashfa ya rada suala ambalo nalo hajalitolea maelezo yoyote. Hadi hivi sasa uchunguzi wetu unaonesha kuwa asilimia 90 ya uamuzi uliofikiwa hadi sasa ni kutoendelea na suala la Dowans.

Hata hivyo upande mwingine bado unadokeza kuwa endapo serikali haitanunua mitambo ya Dowans na hivyo kuwasababishia hasara "wawekezaji" hao ambao walikuwa na uhakika kuwa serikali itanunua mitambo hiyo basi Watanzania "watakiona" kwani upungufu mkubwa wa umeme ambao tulidokeza unakuja mwezi wa nne, utaifanya serikali iipigie magoti Dowans na hata kununua majenereta yale yale katika bei ya juu!!

"Watanzania hawawezi kuvumilia kukaa gizani muda mrefu hasa huku mjini, kwa hiyo usishangae hao hao wanaopinga sasa wakaja baadaye kutaka serikali inunue mitambo hiyo aidha kutoka kwa dowans au kwa mtu atakayekuw ameinunua" alisema mdokezaji huyo.

Uwezekano wa kutokea yote mawili ni mkubwa zaidi. Hata hivyo, kama dhamira ya kuwalipa Dowans kwa gharama yoyote itatekelezwa basi kuna dalili Dr. Idris na timu yake watacheza bahati nasibu na kuendelea na mradi huo wakijua kuwa huko Bungeni tayari wana kura za kutosha kuzuia mapigo ya kina "mwakyembe".
Comments (6)add comment
Longii Tigwa: ...
Huyu bwana akijiuziulu atakuwa amefanya jambo la maana kabisa, mpaka hivi sasa anasimamia maslahi ya dowans na wamiliki wake si maslahi ya watanzania. Ni bora huyu akaondoka mapema kunakila uwezekano wa kutumiwa na hawa dowans na akisukumwa na masilahi aliyonayo kwao akaihujumu tanesco. Ondoka mapema wako watanzania wazalendo kibao wanaoweza kufanya zaidi ya uliyoyafanya hapo tanseco, jackoff.
1

March 05, 2009
Votes: +0
Mfia Nchi: ...
Kwa swala hili kusema kweli kuna mazingira ya kuto kukoma kwa ufisadi nchini. Kama kuna utata kwenye ununuzi wa mitambo hiyo, basi ni wazi haina haja ya kununua, kama kampuni yenyewe iliingia kwa utata kwenye mkataba basi ni moja kwa moja hao ni mafisadi tu.
Jambo la msingi Spika Sita, Mwakyembe na timu yao kama si bunge kwa ujumla waishauri serikali kutafuta mtu makini kwa baraka zote kuleta mitambo mizuri ya kuzalisha umeme. Ili hao DOWANS nao wale hasara wakione cha moto. Badala ya kukaa kubishana kuhusu ununuzi wa mitambo hiyo. Na isijetokea kuwa ni mibovu au ni feki kabisa.
Serikali NUNUENI MITAMBO MIPYA kutoka hata kwa swahiba zenu China, Japani hata Ujeremani
2

March 06, 2009
Votes: +0
MKEREME: ...
Huyu Dr. Rashid hawezi kujiuzulu kwani kazi aliyotumwa kuifanya TANESCO hajamaliza. Mwaka juzi alikopa Billoni 300 kutoka kwa Mabenki aliyochagua mwenyewe akiwa kama Governor wa BOT sasa aulizwe hizo pesa amepeleka wapi. Kwa Mchumi wa kiwango cha darasa la saba( UPE) watu wanakopa pesa kwa ajili ya kuwekeza kwenye mtaji lakini huyu Dr. Idris alikopa akalipa madeni ambayo wala hakujiuliza yalitokana na nini kwa sababu walioshindwa kulipa hakuwakuta.Mabilioni hayo angewaza kununua mitambo ya Megawati 300 na kuganga njaa kungeisha. Ni sawa na kuchukua pesa SACCOS ukalipe chakula na BIA pamoja na kanga ya Mamsapu dukani kwa Mangi.Kabla hajajiuzulu atuambie hizo pesa za madafu ya MaBenki alizo na maslahi binafsi nazo atazilipa vipi pamoja na RIBA huku Shirika likitengeneza hasara ya Billions kila mwaka kwa kuwalipa akina SONGAS ambao ni watu hewa? Au kwa vile ataondoka kama alivyofanya kule BOT na vijsenti vya RADA asiulizwe? Watu wa SYSTEM mnafanya nini ?
Ni BORA bosi wenu wa Kuchomekea aliyepitia kwenye Tanuru la akina Rostam nae atangaze kujiuuzulu
Wizi mtupu. Hata mkiongeza tija na bei ya umeme ikafika unit shillingi 500 /= kwa madeni aliyongezea Dr. Rashid kwa hiyo miaka miwili lazima tanesco iende kuzimu. Akiamaliza mkataba wake wa three years hapo Disemba mwaka huu atakuwa ameliacha shirika ICU .Kuna dalili za kuongezewa watu wapate pesa za Kampeni uchaguzi hauko mabali.Hata ukimpa Bill Gate na WIZARD yake ya Microsoft hawezi kulifufua. Lakaini kwa sababu mwenye hisa 100 ni SERIKALI hawAtakubali life litanusurika at big cost that is for sure. Kuchanganya kiswahili na kizungu nimeiga kwa Ngeleja kwani si tunaongolea Nishati? Lazima nionekane NSHOMOILE bwana. Yetu macho biashara asubuhi jioni mahesabu bwana.
3

March 06, 2009
Votes: +0
dickabudi: ...
Mitambo ya Dowans isinunuliwe wala kuzungumzwa kwani zipo njia nyingi tu za kupata majenereta ya dharura la kwanza likiwa ni kuingia mikataba na waundaji wa mitambo hiyo Marekani na kwingineko duniani yaani Taifa liwasiliane moja kwa moja na Makampuni wa kujenga mitambo sio wakala wa mauzo, muda upo. tukumbuke majenereta yote yaliletwa na ndege za kirusi hivyo hadi April muda upo, iende team ijadili hire purchase, serikali/TANESCO wasign mkataba wa wazi chini ya utaratibu wa INTERNATIONAL SHOPPING na PUBLIC PROCUREMENT under urgency wazingatie uwazi na ukweli
4

March 06, 2009
Votes: +0
Atubonekisye Massapa: ...
Mwanakijiji,
Kwanza Serilikali ilikana kununua mitambo hii. Wajanja wakakaa, wakachora dili.
Ghafla Barrick wanajitoa kwenye mradi wa gesi, hivyo wanacreate "shock" kwa Serikali.
Mabingwa wa hesabu wanakuja na hitimisho: shortage ya umeme. Halafu wanakaa na Idrissa, wanampiga shule. Anakuja na dili. Linawekwa mezani. Waziri wetu anaruka juu :YEP! Here they are! Done
Wanajua sana waropokaji, wanamwita Zitto: Hoji ya IPTL. Naye kwa upofu wa ufisadi Anajikwa......

Inatisha.Serikali iache uvivu, idhamini yenyewe miradi ya kitaifa kama wanavyofanya Rwanda, hii tisha nyani itaisha. Na Ole wao wa create ARTIFICIAL Power shortage, tutawa "audit kujua shortage ya umeme wakati wa masika!!!
5

March 06, 2009
Votes: +0
londa: ...
waachiwe tanesco kuamua what is right siyo wanasiasa .....kwa hili wanasiasa wanatafuta umaarufu zaidi kuliko hali halisi na utaalamu...my position is
1. Kuwasikliza wataalamu wa Tanesco wanashauri nini! na kwanini yaani what is pro and cons of each available alternatives
2. Watuambie njia zipi tofauti zilizopo na hasara na faid yake yaanike hadharani halafu sisi tutawasidai kutoa input zetu
3. Kutishia kujiuzulu ni kutishia nyau....akitaka anaondoka hatokosi MD or DG wa tanesco kama tuliweza kuwa net group pronlem na kuwalipa for all those year why not now!
4. Evalasting solutions must be in place sio habari ya solution ya muda mfupi...
6

March 07, 2009
Votes: +0

Write comment

busy
Last Updated ( Friday, 06 March 2009 )
 
Ni nani anafaa kuingoza Tanzania kama Rais kuanzia 2010-2015?
 

Photo Albums

Just $6.95/Mo
Unlimited Space, Unlimited Transfer, Free Domain
www.bluehost.com

MwanaKijiji.COM LIVE

Window Player   RealAudioPlayer   Itune Player