|
Programu za maendeleo au ulaji? |
|
Written by M.M. Mwanakijiji
|
|
Tuesday, 07 April 2009 |
Kuna miradi mbalimbali ambayo inatekelezwa/itatekelezwa na wizara mbalimbali na taasisi mbalimbali kwa mwaka huu wa fedha. Ukipata nafasi ya kupitia taarifa hiyo ya mipango mbalimbali ya serikali utaweza kuona jinsi gani wakubwa wa nchi yetu wanavyojua jinsi ya kugawa fedha kwa kufuata “kipaumbele”. Utagundua mara moja kuwa tatizo la Tanzania siyo fedha! Kuna tatizo kubwa zaidi ambalo ni vigumu kuliondoa.
Mojawapo ni mradi wa “Deepening Democracy in Tanzania Program”. Mradi huu umetengewa fedha nyingi katika sehemu tatu:
Fedha zilizotengwa kwa ajili ya mradi huu (unatakiwa kutekelezwa mwaka huu wa 2008/2009) ziko hivi:
Msajili wa Vyama vya Siasa: zimetengwa kiasi cha Tsh 178,954,200 Mfuko wa Bunge: 355,232,900 Tume ya Uchaguzi: 596,362,400
Taarifa zenyewe ziko kwenye forums, upande wa Uchumi. Kumbuka kuwa mipango hii inaandaliwa wakati ule ule wa bajeti? Ina maana gani kwenye suala la Dowans?  Swali jingine: What on the earth is going on? Do these people have short memories or selective memories? Or beside not having very good lawyers probably we don't have very good planners either? M.M.
|
|
Last Updated ( Tuesday, 07 April 2009 )
|