Tumepiga kelele kwa miaka minne na kelele zetu zimebatizwa kuwa ni "chuki binafsi". Tumewapigia mbiu waamke lakini panda zetu zimekuwa ni "kelele za mlango" ambazo hazimzuii mwenye nyumba kulala. Tumesema mfumo wa utawala wa kifisadi nchini ni matokeo ya utawala wa CCM, wakatuambia kuwa 'ufisadi ni wa mtu mmoja mmoja na siyo chama". Wengine wakathubutu kutuambia kabisa kuwa "mafisadi ndani ya CCM ni wanne na wamefikishwa mahakamani". Tumesema ufisadi ni matunda na mazao ya utawala wa CCM na watu wengine wanasema tumefanya hivyo kwa sababu tuna &qu...