JIJI la Tanga limfeunikwa na simamzi kuu kufatia wanafunzi 18 wa Chuo cha Kiislamu cha Shamsil-Maariff kufa papo hapo na wengine 125 kujeruhiwa vibaya, baada ya lori walilokuwa wakisafiria kutoka kwenye sherehe za maulidi kupinduka. Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Adolphina Kapufi aliliambia gazeti hli jana kuwa ajali hiyo ilitokea saa 5:30 usiku wa kuamkia jana katika eneo la njiapanda kuu ya Mabanda ya Papa jijini hapa. Kapufi aliwataja baadhi ya waliokufa katika ajali hiyo kuwa ni Twalib Kunemu, Juma Idd, Faraji Habib, Jahshi Rashid, Hussein Bakari, Hajji Athumani naYus...