MwanaKijiji.COM

Wednesday
Feb 08th
Text size
  • Increase font size
  • Default font size
  • Decrease font size
Home arrow LifeStyle arrow Maisha arrow Aliyempiga picha ya uchi mtoto wa shule adai "nilipitiwa na shetani"
Aliyempiga picha ya uchi mtoto wa shule adai "nilipitiwa na shetani"
(10 votes)
Written by M. M. Mwanakijiji   
Wednesday, 12 August 2009
lifestyleASKARI anayetuhumiwa kuwapiga picha za uchi mwanafunzi wa Shule ya Msingi Kurasini Dar es Salaam na mama mjamzito mwishoni mwa wiki amejitokeza na kukiri kosa na kuwaomba radhi walalamikaji kwa maelezo kwamba alipitiwa na shetani. Akizungumza na gazeti hili jana kituo cha Polisi Barabara ya Kilwa askari huyo alisema alikifanya kitendo hicho  kwa bahati mbaya na hakuwa na nia yoyote ile mbaya kwa mwanafunzi huyo na mjamzito huyo. "Sikuwa na nia mbaya ila shetani tu aliyenipitia hivyo nawaomba walalamikaji wangu anisamehee kwa yote yaliyotokea, nipo tayari tulizungumze kiubinadamu."alisema askari huyo.

Katika hatua nyingine, mama mzazi wa mwanafunzi huyo Bi. Bernadeta Fatael mbaye alifika kituoni hapo kwa mara ya kwanza tangu kutokea tukio hilo, alisema siku hiyo  hakuwepo alikuwa katika mihangaiko yake

Alisema kuwa kutokana na baba mkubwa wa mwanafunzi huyo kwenda kazini jana ilimlazimu  kwenda kituoni hapo ili kujua hatima ya kesi hiyo.

Bi. Bernadeta, alisema kuwa baada ya kufika kituoni hapo  mpelelezi wa kesi yao alimwambia kuwa asubiri kidogo ili naye aende kutoa maelezo yake.

"Muda kidogo waliniita ndani nilipoingia waliniuliza jina langi kisha kuanza kunihoji na walipomaliza waliniambia niweke saini karatasi ile,"alisema.

Kabla ya kutia saini alimuomba mpelelezi huyo kumsomea ili ajue nini kilichoandikwa.

"Mwanzo wa maelezo alisoma kile alichokuwa ananihoji lakini mwishoni nilishituka baada ya kuandika kuwa nikiwa kama mwakilishi wa upande wa wazazi tulikaa na kuafikiana kumsamehe askari huyo kitu ambacho sikukisema,"alisema mama huyo.

Baada ya kugundua njama hizo alimuita mlalamikaji mwingine ambaye mke wake naye alipigwa picha hizo, Bw. Frank Kazimili ambapo alimwambia askari huyo kitendo anachotaka kukifanya ni kinyume na sheria na ni njama  za kutaka kumsaidia askari huyo.

"Haiwezekani kabisa kwa nini amuite huyu mama pekee yake wakati walalamikaji wote tupo hapa na kitendo cha kutaka kumsainisha bila kutushirikisha na kusema kuwa tumemtuma sisi kama walalamikaji kuwa tumefikia muafaka wa tunamsamehe ni uongo na mpelelezi huyu hatumtaki hatuna imani naye,"alisema Bw. Kazimili.
 
Comments (4)add comment
Agnes: ...
Hivi jamani kweli dunia inakaribia mwisho,huyu askari alikosa kabisa kazi ya kufanya hata kwenda mazoezi mpaka akapata ushawishi mbaya,jama tubadilike na inabidi apewe adhabu walau ya mfano ili kitendo kama hiki kisije jirudia
1

August 14, 2009
Votes: +0
Mapuchila: ...
sas wakati umefika wa serikali kufikiri upya ni sifa gani hasa zitumike kuajiri polisi.Huyu polisi aliyefanya unyama huo,ndiyo ni unyama anakipaji kupiga picha n a si kulinda raia na mali zao.sikweli kwamba alipitiwa na ilikuwa bahati mbaya.Tunataka sheria ichue mkondo wake na haki itendeke ili iwe fundishon kwa wengine.
2

August 17, 2009
Votes: +1
Babalao: ...
du !! dunia ina mambo kweli, na huyu shetani ambaye kila kukicha anawakosesha, kiama chake kikifika, dunia itauwa paradiso
3

May 23, 2010
Votes: +1
ABUBAKARI: ...
NINACHOTAKA KUSEMA NI KWAMBA HATUELEWI MAZINGIRA YA TUKIO. MPAKA HUYO ASKARI ANAPIGA PICHA ILIKUWAJE. INAWEZEKANA HAO NI WAPENZI WA MUDA MREFU. KWAHIYO WMEKUBALIANA AMPIGE PICHA SEHEMU ZAKE ZA SIRI. SI HATUWEZI JUA. WAMEPENDANA WENYEWE WWANAPEANA MALAVIDAVI. WAACHENI WASTAREHE. SIYEYE WAKWANZA KUPIGWA PICHA ZA UCHI. ILA KOSA MAPAPARAZI WAMEZIKAMATA.
4

January 27, 2011
Votes: +2

Write comment

busy
 
Ni nani anafaa kuingoza Tanzania kama Rais kuanzia 2010-2015?
 

Photo Albums

Just $6.95/Mo
Unlimited Space, Unlimited Transfer, Free Domain
www.bluehost.com

MwanaKijiji.COM LIVE

Window Player   RealAudioPlayer   Itune Player