MwanaKijiji.COM

Monday
May 21st
Text size
  • Increase font size
  • Default font size
  • Decrease font size
Home arrow National arrow Coastal Zone arrow Sumatra yawapandishia nauli wanafunzi wa sekondari
Sumatra yawapandishia nauli wanafunzi wa sekondari
(0 votes)
Written by Tanzania Daima   
Thursday, 06 November 2008

Usafiri MbovuMAMLAKA ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra), inatarajiwa kupandisha nauli kwa wanafunzi wa shule za sekondari kwa kuwataka kulipa nusu ya nauli ya mtu mzima.

Hayo yalibainishwa jana na Rais wa Umoja wa Wanafunzi wa Shule za Sekondari Taifa, Silvester Kijingo, alipozungumza na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Dar es Salaam.

Alisema Sumatra imewaandikia barua na kuwajulisha kupanda kwa nauli hiyo kuanzia Julai mwakani na kusema kwamba nauli ya mwanafunzi wa shule ya msingi itaendelea kubaki sh 100.

Rais wa wanafunzi hao, alisema licha ya Sumatra kuwaandikia barua hiyo, lakini mpaka sasa wao kama wanafunzi hawana tamko lolote hadi hapo watakapowashirikisha wadau mwengine.

Alisema tatizo la nauli limekuwa kero kwao, lakini kipindi hiki wanataka ikifikie muafaka mzuri katika nauli za daladala na hata zile za mkoani na mjadala huo wa nauli watauibua baada ya kumaliza uchaguzi wa Rais katika shule za sekondari taifa.

Kijingo alieleza licha ya Sumatra kuwaruhusu wanafunzi kukaa kwenye viti kutokana na kulipa nauli ya sh 100, lakini tatizo bado lipo hasa kwa wanafunzi wa kike ambao wanakaa mbali na kupanda daladala zaidi ya moja.

“Lakini kuna wanafunzi wengine wanadandia malori ya mchanga na hawa ni wale wanaokaa mbali tena wanaishi katika mazingira magumu…na matokeo yake wanafunzi wengi ndoto zao zinapotea hasa pale wanapopewa ujauzito na hao madereva,” alisema Kijingo.

Comments (0)add comment

Write comment

busy
Last Updated ( Thursday, 06 November 2008 )
 
Ni nani anafaa kuingoza Tanzania kama Rais kuanzia 2010-2015?
 

Photo Albums

Just $6.95/Mo
Unlimited Space, Unlimited Transfer, Free Domain
www.bluehost.com

MwanaKijiji.COM LIVE

Window Player   RealAudioPlayer   Itune Player