MwanaKijiji.COM

Friday
Jul 30th
Text size
  • Increase font size
  • Default font size
  • Decrease font size
Home arrow National arrow Lake Zone arrow Masha awakwepa albino Mwanza?
Masha awakwepa albino Mwanza?
(0 votes)
Written by Nipashe   
Monday, 10 August 2009

Maalbino wamewataka Waziri wa Mambo ya Ndani, Laurence Masha na Mbunge wa Ukerewe, Getrude Mongella, kumrejea Mungu kutokana na kudaiwa kuwalaghai. Shutuma hizo zilitolewa na wanachama wa Chama cha Albino Mkoa wa Mwanza (TAS), walipotembelewa na waandishi wa habari. Mwenyekiti wa Tas, Alfredy Kapole, alisema Masha amekuwa akitoa matamko ya kulinda albino wakati hata idadi yao walioko Mwanza haijui.

Kapole alisema hajawahi kukutana na Waziri wala Mbunge licha yao kumtafuta anapokuwa ziarani mkoani hapa na kuahidi angefika bila kutimiza ahadi au kutoa taarifa ya udhuru na kwamba, wanamweka kwenye orodha ya wanaowanyanyapaa.

"Tunalia kila siku na serikali yetu kutokujali maana waziri ambaye mkoa wake unaongoza kwa mauaji ya albino tunamuomba kukutana naye anatuahidi kisha anadharau, huyu kweli anaguswa na matatizo yetu?" alihoji Kapole.

Pia, alisema Masha kama mbunge hakuwahi kuwatembelea wala kuwasikiliza jinsi wafanyavyo wabunge wengine na kwamba kitendo hicho kinawasikitisha kuona mtu aliye na dhamana anashindwa kutimiza wajibu wake

"Mbona alikwenda Tarime wakati wa mapigano, lakini tulioko hapa licha ya kuomba tuongee alitupuuza, hivi kweli viongozi wetu hawa wanatekeleza utawala bora?" alihoji.

Kuhusu Mongella alisema uchaguzi wa mwaka 2005, alijinadi jimboni kwake Ukerewe kwa kuahidi kuwa akichaguliwa atawajengea kituo maalum. "Hawa wanasiasa nia yao ni kupata kura kupitia watu wenye matatizo wakipata hawarudi...hili ni tatizo la kufa nafsi zao wanatakiwa kumrudia Mungu," alisema.

Alisema albino 16 wameuawa mkoani hapa tangu mwaka 2006, huku wawili wakipotea, mmoja kujeruhiwa na makaburi sita yalifukuliwa.

CHANZO: NIPASHE
Comments (0)add comment

Write comment

busy
 
Just $6.95/Mo
Unlimited Space, Unlimited Transfer, Free Domain
www.bluehost.com

MwanaKijiji.COM LIVE

Window Player   RealAudioPlayer   Itune Player