|
Moto kituo cha Mafuta Mwanza wazimwa |
|
Written by Mwanakijiji
|
|
Monday, 27 October 2008 |
Vikosi vya zimamoto na wananchi wa mji wa Mwanza wakiongozwa na Mkuu wa Polisi wa Mkoa huyo Bw. Rwambow wamefanikiwa kuzima moto mkubwa uliotokea kwenye kituo cha mafuta kilichoko barabara ya Nyerere mjini Mwanza (pichani). Hadi sasa hivi habari za awali zinasema mtu mmoja amefariki na mali yenye thamani ya mamilioni ya shilingi kuteketezwa. (Updated 11:30AM) Moto huo ulitokea kwenyekituo cha mafuta cha MOIL kilichopo kwenye maungano ya Barabara ya Nyerere na Pamba mjini hapo majira ya saa moja na nusu za jioni. Ajali hiyo inadaiwa imetokana na lori moja ambalo lilikuwa limebeba magodoro na bidhaa nyingine kufika kituoni hapo (pichan) kwa ajili ya kujaza mafuta. Haijajulikana hasa ni nini kilichosababisha moto huo lakini yawezekana "kichungi cha sigara" kilitupwa eneo hilo na kusababisha lori hilo kulipuka. Vikosi vya uokoaji vilivyofika eneo hilo vinadaiwa vilikuja na maji ya kawaida ambayo hayastahili kuzima moto unaotokana na mafuta.
Kwa mujibu wa chanzo chetu eneo la tukio, ilikuwa ni juhudi ya vijana waliokuwa eneo hilo kutumia mchanga mbichi ulioletwa na lori ndipo moto uliweza kuzimwa baada ya vikosi vya zima moto "kwenda na kurudi" kuleta maji ya kawaida na kuhangaika na uzimaji wa moto huo kwa karibu masaa mawili. Hata hivyo hadi walipofanikiwa kuzima moto huo sehemu ya kituo hicho ilikuwa imeteketea kabisa. Kituo hicho ni kile kinachomilikiwa na Mansour mfanyabiashara ambaye pia anadaiwa kutaka kununua uwanja wa Nyamagana. Hadi hivi sasa habari ambazo hazijathibitishwa zinasema kuwa mtu mmoja amefariki dunia katika moto huo mkali wa mafuta.
|
|
Last Updated ( Tuesday, 04 November 2008 )
|