MwanaKijiji.COM

Wednesday
Feb 08th
Text size
  • Increase font size
  • Default font size
  • Decrease font size
Home arrow National arrow Lake Zone arrow Polisi yatangaza vita na majambazi
Polisi yatangaza vita na majambazi
(1 vote)
Written by Tanzania Daima   
Monday, 03 November 2008

Mwanza-JESHI la Polisi mkoani Mwanza, limetangaza vita dhidi ya Watanzania na raia wanaotoka nchi jirani na kujihusisha na vitendo vya ujambazi, wilayani Geita, mkoani hapa na kwamba litaanza kuwashukia kama mwewe kwenye vifaranga wa kuku.

Jeshi hilo limesema limejiandaa kukabiliana na vitendo hivyo vya ujambazi, ambavyo vimekuwa vikitokea mara kwa mara wilayani Geita na kuhatarisha usalama wa raia na mali zao.

Vita hiyo ilitangazwa jana na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mwanza, Jamal Rwambow (RPC), wakati akizungumza na viongozi na watendaji wa halmashauri ya wilaya hiyo, katika kikao cha Baraza la Madiwani.

Mbali na hayo, kamanda huyo ametangaza pia kuwafukuza kazi askari wote watakaobainika kushirikiana na majambazi au kwenda kinyume cha taratibu na kanuni za jeshi hilo.

“Nimeandaa utaratibu wa kuwanasa majambazi na askari watakaoonekana kujihusisha na kushirikiana na watu kama hao, ikiwa ni shabaha halisi ya kutokomeza kabisa vitendo hivyo na kusafisha harufu mbaya iliyojengeka kwa jeshi hilo,” alisema.

Kamanda Rwambow alisema Wilaya ya Geita, imekuwa na historia mbaya kwake kwani vitendo vya ujambazi vimeonekana kukithiri mara tu baada ya kuhamishiwa yeye mkoani hapa.

“Nilipohamishiwa Mwanza, Geita ilinipokea vibaya sana, matukio ya ujambazi yalijitokeza kwa kasi na nguvu kubwa na hadi sasa vitendo vya ujambazi katika wilaya hii bado vipo, tena sana.

“Kutokana na ukweli huo, mimi na jeshi langu nimejipanga vizuri kupambana na majambazi haya…..hakika vita hii haitanishinda hata kidogo, nimedhamiria kukomesha hali hii, uwezo ninao na nia ipo,” alisema RPC Rwambow.

Kuhusu hilo, aliwataka viongozi, watendaji wakiwemo madiwani na wakazi wa wilaya hiyo, kushirikiana vema na jeshi hilo katika kupambana na ujambazi wilayani humo.

Kwa mujibu wa kamanda huyo wa polisi, utoaji taarifa za siri kwa jeshi hilo ni miongoni mwa njia zitakazoliwezesha jeshi hilo kushinda kwa urahisi vita hiyo na kwamba kamwe hataridhia kuona wakazi wa Wilaya ya Geita na mkoa kwa ujumla, wakiishi kwa kuhofia usalama wa maisha na mali zao.

“Polisi imekamilika kila idara na hizi ni salamu kwa haya majambazi…..sitakubali mkoa wangu uyumbishwe na watu wachache, la hasha! Kikubwa, nawaombeni viongozi, watendaji na madiwani pamoja na wananchi, tupeni taarifa tuzifanyie kazi,” alisema Kamanda Rwambow.

Kwa upande wao, madiwani na wakuu wa idara wa halmashauri hiyo walieleza kusikitishwa kwao na uonevu unaofanywa na Jeshi la Polisi wilayani humo kupitia askari wake.

Walisema, mara yanapotokea matukio ya ujambazi wilayani humo, polisi wamekuwa wakishindwa kukabiliana na majambazi, badala yake wanaanza kukamata raia wema bila kosa na sababu zozote, ili wapewe hongo.

“Tumekusikiliza kamanda wetu wa polisi! Lakini mbona askari wako wa wilaya hii wamekuwa wakikamata raia wasiokuwa na hatia, badala ya wale wanaojihusisha na vitendo vya ujambazi?.

“Watu wamekuwa wakikamatwa ovyo na kuombwa fedha, hivi hii ndiyo falsafa ya Jeshi la Polisi? Tunaomba uwamulike askari wako wa wilaya hii na ikiwezekana uwahamishe, kwani baadhi yao wapo hapa tangu miaka ya 80,” alisema John Magulu, diwani wa Kata ya Bukondo.

Comments (0)add comment

Write comment

busy
Last Updated ( Monday, 03 November 2008 )
 
Ni nani anafaa kuingoza Tanzania kama Rais kuanzia 2010-2015?
 

Photo Albums

Just $6.95/Mo
Unlimited Space, Unlimited Transfer, Free Domain
www.bluehost.com

MwanaKijiji.COM LIVE

Window Player   RealAudioPlayer   Itune Player