MwanaKijiji.COM

Wednesday
Feb 08th
Text size
  • Increase font size
  • Default font size
  • Decrease font size
Home arrow National arrow Lake Zone arrow Walinzi washikiliwa kwa kushirikiana na majambazi kuvamia mgodi
Walinzi washikiliwa kwa kushirikiana na majambazi kuvamia mgodi
(0 votes)
Written by Habari Leo   
Wednesday, 14 January 2009
Polisi mkoani Shinyanga inawashikilia walinzi wawili wa Kampuni ya kuchimba Almasi ya El-Hilal kwa tuhuma za kushirikiana na majambazi kuvamia mgodi kwa kutumia silaha.

Taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Shaibu Mohamed inasema walinzi hao Amos Joseph (24) mkazi wa Mwadui na Thomas Mipawa (30) mkazi wa Kishapu wanaonekana kushiriki katika tukio la ujambazi katika mgodi huo lililofanyika Jumatatu usiku.

Mohamed alisema siku ya tukio watu wapatao saba wakiwa na silaha walimweka chini ya ulinzi Amos na kumnyanganya silaha aina ya shotgun yenye namba Mv 03727 mali ya kampuni hiyo ya mgodi.

Alisema baada ya polisi kufanya msako katika pori linalozunguka chumba cha kuchambulia almasi walikamata bunduki aliyokuwa amenyang’anywa mlinzi huyo ikiwa imefichwa na majambazi kwa lengo la kuirudia baadaye.

Uchunguzi kuhusu tukio hilo unaendelea ili kuwafikisha mahakamani. Katika tukio jingine, watu wanaodhaniwa kuwa majambazi, wamemvamia Mabala Chongela (37) na kumpora Sh 150,000, simu ya mkononi.
Comments (0)add comment

Write comment

busy
 
Ni nani anafaa kuingoza Tanzania kama Rais kuanzia 2010-2015?
 

Photo Albums

Just $6.95/Mo
Unlimited Space, Unlimited Transfer, Free Domain
www.bluehost.com

MwanaKijiji.COM LIVE

Window Player   RealAudioPlayer   Itune Player