MwanaKijiji.COM

Wednesday
Feb 08th
Text size
  • Increase font size
  • Default font size
  • Decrease font size
Home arrow National arrow Lake Zone arrow Wauawa kwa tuhuma za kuiba ng’ombe
Wauawa kwa tuhuma za kuiba ng’ombe
(0 votes)
Written by Habari Leo   
Wednesday, 14 January 2009
Watu watatu wamefariki dunia wilayani hapa baada ya kushambuliwa na kundi la wananchi wakituhumiwa kuiba ng’ombe na kisha kuwachinja. Tukio hilo lilitokea jana katika kijiji cha Nyakaduha, Kata ya Lubanga Tarafa ya Kasamwa.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mwanza, Jamal Rwambow, aliwataja watuhumiwa kuwa ni Samwel Delebi (32)mkazi wa kijiji cha Kamhanga, Charles Lufingilo (35) mkazi wa kijiji cha Nyakaduha na Daud Misungwi (32) mkazi wa kijiji cha Isegenge wilayani Sengerema.

Akisimulia mkasa huo, Kamanda Rwambow alisema kuwa watuhumiwa hao wanadaiwa kuhusika katika wizi wa kundi la ng’ombe uliotokea katika kijiji cha Kamhanga, ambapo baada ya wizi huo wananchi wa kijiji hicho walipiga mayowe na kuanza kufuatilia. Baada ya wizi huo, waliwachinja ng’ombe na kuanza kuuza nyama kwenye miji mbalimbali walipokuwa wakipita huku wakitafuta soko la wale wengine waliokuwa hai.

Kamanda Rwambow alionya tabia ya wananchi kujichukulia sheria mikononi kwa kuwaua watuhumiwa. Wakati huo huo kutoka Sumbawanga, Gurian Adolf anaripoti kwamba watu wawili wamekufa katika matukio tofauti likiwemo la mmoja kuuawa kwa kupigwa na wananchi wanaodaiwa kuwa na hasira kali wakimtuhumu kwa wizi wa magunia mawili ya mahindi.

Evod Kipaila (50) mkazi wa kijiji hicho, aliuawa kwa kipigo na wananchi kwa madai kuwa aliiba magunia mawili ya mahindi yenye thamani ya Sh 54,000. Kifo kingine ni cha Hassan Abel (30) mkazi wa kijiji cha Ipwaga katika makazi ya wakimbizi ya Mishamo wilayani Mpanda ameuawa na watu wasiofahamika na kisha maiti yake kuitelekeza barabarani.
Comments (0)add comment

Write comment

busy
 
Ni nani anafaa kuingoza Tanzania kama Rais kuanzia 2010-2015?
 

Photo Albums

Just $6.95/Mo
Unlimited Space, Unlimited Transfer, Free Domain
www.bluehost.com

MwanaKijiji.COM LIVE

Window Player   RealAudioPlayer   Itune Player