MwanaKijiji.COM

Wednesday
Mar 10th
Text size
  • Increase font size
  • Default font size
  • Decrease font size
Home arrow NEWS arrow Taifa arrow Kampeni ya kuwasaidia wahanga wa mafuriko yaanza!
Kampeni ya kuwasaidia wahanga wa mafuriko yaanza!
(0 votes)
Written by M. M. Mwanakijiji   
Sunday, 10 January 2010
Breaking NewsSiku ya Jumamosi tumepata nafasi ya kuzungumza na Mkurugenzi wa Idara ya Maafa ya Chama cha Msalaba Mwekundu Bw. Joseph Kimaryo kuhusu hali ya wahanga wa mafuriko ambayo yameikumba nchi yetu. Unaweza kusikiliza mahojiano haya na kupata nakala ya jinsi ya kusaidia ndugu zetu hawa ukibonyeza ili kusoma zaidi hapa.
Unaweza kupata mpango tulio nao hadi hivi sasa wa kushiriki katika kuchangia wahanga wa mafuriko yanayoendelea nchini kupitia Chama cha Msalaba Mwekundu. Tumepata nafasi ya kuzungumza kwa kirefu na Mkuu wa Kitengo cha Maafa wa chama hicho nchini Bw. Joseph Kimaryo ambaye anatueleza hali ilivyo hadi hivi sasa (Jumamosi Januari 9, 2010).


Kwa kushirikiana na tovuti za Jamiiforums na Mdau wa Jamii Bw. Issa Michuzi; pamoja na kushirikiana na Mtandao wa Wanaataluma wa Tanzania (TPN) tumeandaa mpango wa kuwashirikisha Watanzania mahali popote pale walipo kuchangia katika adha hii inayowakuta ndugu zetu katika mikoa mbalimbali hasa Morogoro, Dodoma, na sasa hivi Shinyanga na hata Mwanza na kuna uwezekano wa sehemu nyingine nchini kwa kadiri siku zinavyoendelea.

Tumeamua kutumia Chama cha Msalaba na Mwezi Mwekundu cha Tanzania kwani rekodi yao katika kufika na kutoa misaada wakati wa majanga hailinganishwi na chombo au taasisi nyingine yoyote. Zaidi ya yote tumepata uhakika wa kutosha wa misaada yetu kufika kwa walengwa baada ya kuzungumza na Katibu Mkuu wa Chama hicho Mstahiki Meya (Dar) Adam Kimbisa (CCM).

Pata nakala ya mpango huo hapa:
http://www.box.net/shared/g99no7hjkg

Sikiliza mahojiano online:
BONYEZA HAPA

Au download kutoka hapa:
http://www.box.net/shared/8v7o0thdvt
Comments (1)add comment
Kama: ...
Heri ya mwaka mpya Mwanakijiji!!!!

Sasa mwanakijiji tutawezaje kuchangia pesa iwapo hapa tunapotoa maoni tulio wengi miongoni mwetu hatutumii majina yetu halisi na bila kufahamika kwa sababu ambazo zinazopekelea sisi kujificha bado zina-exist na tunashindwa kujitokeza hadharani kwa majina yetu halisi. Hauoni kama hicho ni kitendawili mpiganaji mwenzetu.
1

January 12, 2010
Votes: +1

Write comment

busy
Last Updated ( Sunday, 10 January 2010 )
 
Just $6.95/Mo
Unlimited Space, Unlimited Transfer, Free Domain
www.bluehost.com

MwanaKijiji.COM LIVE

Window Player   RealAudioPlayer   Itune Player