Aliyekuwa Mhadhiri Mwandamizi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Issa Shivji, amewatuhumu baadhi ya wawekezaji wa sasa nchini kuwa ni wabakaji na wanyanganyi wa rasilimali za Tanzania. Profesa Shivji alikuwa akichangia mada wakati wa kongamano la siku tatu lililohitimishwa jana lililokuwa likijadili mustakabali wa Tanzania, katika kumbukumbu ya miaka kumi ya tangu kifo cha Mwalimu Julius Nyerere. Akasema wawekezaji wa sasa, hasa katika taasisi nyingi za kifedha zimekuwa kama mchezo wa pata potea.