JAJI Mkuu wa Tanzania Augustine Ramadhani, amesema ametumia fedha zilizotengwa kwa ajili ya ukarabati wa nyumba anayotakiwa kuishi kumalizia ujenzi wa Jengo la Utawala la Mahakama ya Rufani. Akizungumza wakati wa hafla ya kuzindua jengo hilo ambalo pia linatumika kama kumbukumbu ya Jaji Mkuu wa kwanza mzalendo Augustine Said jana Dar es Salaam, Jaji Mkuu alisema hakuona umuhimu kufanya ukarabati wa nyumba ya Jaji Mkuu na badala yake kuitumia kwa ajili ya kumalizia jengo hilo kwa manufaa ya taifa.
“Niliamua kulipa jengo hili umuhimu kuliko kukarabati jengo la Jaji Mkuu, na kwa maana hiyo nitakuwa jaji wa kwanza ninayeishi kajificheni,” alisema Jaji Ramadhani na kuongeza kuwa jengo hilo limejengwa kwa thamani ya Sh bilioni 1.3, na pia kutengenezwa sanamu yenye taswira ya mwasisi huyo aliyefariki Aprili 19, 1994. Alisema wameamua kutumia jengo hilo kama kumbukumbu ya mwasisi huyo wa kwanza mzalendo kutokana na ukweli kuwa katika fani ya uanasheria haina utamaduni wa kuwaenzi waasisi wake kama ilivyo katika siasa na kwamba kupitia muasisi huyo, huo utakuwa ndio mwanzo wa kuanzishwa rasmi utamaduni huo. Naye Waziri Mkuu Mizengo Pinda aliyekuwa mgeni rasmi katika shughuli hiyo, alisema wakati umefika kwa viongozi nchini kuachana na dhana ya kikoloni ya kuanza kujinufaisha wenyewe kwanza ndipo wawajali wananchi kwa kuwa dhana hiyo haina ukweli wowote na imejikita katika ubinafsi na uonevu. “Ninasema haya kwa kuwa sasa ninaelewa kuhusu matatizo ya maendeleo ya nchi yetu, katika karne ya 19 kuliibuka dhana ambao wanazuoni tulidhani ni nzuri…ilikuwa inasema maendeleo yatakuja lakini lazima kiongozi atosheke ndio awasaidie wengine,” alisema Pinda. Alisema dhana hiyo haina ukweli wowote na ilitumiwa na wakoloni wakati huo kuhalalisha matendo yao. “Wakati mwingine hata kwa viongozi wetu ni vyema kujinyima ili wananchi wao wafaidi japokuwa inataka moyo lakini ni jambo jema na heshima kwa jamii inayokuzunguka.” Alitoa kauli hiyo kufuatia taarifa kwamba Jaji Mkuu wa Tanzania Augustine Ramadhani, kutumia fedha za kukarabati nyumba yake aliyopangiwa kujengea jengo hilo kwa ajili ya matumizi ya ofisi ya Mahakama ya Rufani na ambalo linatumika kama kumbukumbu ya Jaji Mkuu mzalendo wa kwanza Saidi. Naye Jaji Luis Makame ambaye ni Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, akizungumzia wasifu wa Jaji Saidi ambaye alifanya naye kazi, akiwa kama Jaji Mkuu wa kwanza mzalendo mwaka 1972 hadi 1977, alisema jaji huyo alikuwa akijali sana mambo yanayohusiana na Mahakama. Alisema ndiye alihamasisha mpaka idara inayohusiana na masuala ya mali ndani ya ndoa kuwatambua wanawake ambapo hapo awali idara na sheria zilizokuwapo ziliegemea zaidi kwa upande wa mwanamume. Naye mtoto wa nne wa Jaji Saidi, Daniel Saidi akizungumza kwa niaba ya familia, aliushukuru uongozi wa Mahakama na Serikali ya Awamu ya Nne kwa kumpatia heshima baba yao ambapo atakumbukwa hadi vizazi vijavyo. Picha na Mroki Mroki Pinda azindua jengo la Mahakama ya Rufaa Tanzania Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizindua jengo la kumbukumbu ya Jaji Mkuu wa Kwanza Mzalendo, Hayati Augustine Said kwenye mahakama ya Rufani jijini Dar es salaam March 5, 2010. Wapili kulia ni Jaji Mkuu, Augustine Ramadhan, kulia ni Jaji Kiongozi , Fakihi Jundu.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akikata utepe kuzidua jengo la kumbukumbu ya Jaji Mkuu wa Kwanza Mzalendo, Hayati Augustine Said kwenye mahakama ya Rufani jijini Dar es salaam March 5, 2010. Wapili kushoto ni Jaji Mkuu, Augustine Ramadhan, kushoto ni Jaji Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Jaji Mkuu wa Tanzania Augustine Ramadhan (kushoto) kabla ya kuzidua jengo la kumbukumbu ya Jaji Mkuu wa Kwanza Mzalendo, Hayati Augustine Said kwenye mahakama ya Rufani jijini Dar es salaam. Kiongozi , Fakihi Jundu.My Take: In context the newly built house of the Governor of Bank of Tanzania cost 1.6 Billion Tanzanian Shillings. Do we have our priorities straight? Don't we see something wrong that the Chief Justice refuse to spend a billion shilling to renovate his house instead he chose to build this new building? How can a government allocate money to renovate the house instead of buidling a much needed office building like this one?
|