MwanaKijiji.COM

Monday
May 21st
Text size
  • Increase font size
  • Default font size
  • Decrease font size
Home arrow National arrow Kashfa ATC: Wakodisha Airbus Mbovu kwa Milioni 30 USD
Kashfa ATC: Wakodisha Airbus Mbovu kwa Milioni 30 USD
(0 votes)
Written by Mwandishi Maalum   
Wednesday, 30 January 2008
Article Index
Kashfa ATC: Wakodisha Airbus Mbovu kwa Milioni 30 USD
Page 2
Page 3
Kama vile kashfa ya mahujaji haikutosha, na kama vile mlolongo wa kashfa za manunuzi mengine ya taasisi mbalimbali za serikali hazijaitosheleza serikali ya CCM, shirika la ndege la Tanzania (ATCL) hatimaye nalo limeanza kugubikwa na kashfa kubwa mbili ambazo zimeanza kufukuta pole pole kwa miezi kadhaa sasa.

Kashfa hizo ya kwanza ni ile ya ukodishaji wa ndege kubwa aina ya Airbus 320 MSN 630 (pichani) kutoka kampuni ya Wallis Trading Inc., ya Liberia nchi ambayo miaka michache iliyopita ilikuwa imejikita katika vita vya wenyewe kwa wenyewe. Ndege hiyo kubwa ina uwezo wa kuchukua abiria zaidi ya 150.

 

Matengenezo hayo makubwa ya kuipendezesha ndege hiyo yamefanyika kama magari yanavyofanywa kwenye onesho la  kipindi maarufu cha “Pimp my ride” cha msanii wa Kimarekani Exhibit.  Mara nyingi matengenezo kama hayo hugharimu zaidi kuliko thamani ya kununua gari jipya.

 

Katika jitihada za kulifufua shirika letu la ndege la ATC ambalo lilidorora chini ya uongozi wa waendeshaji toka Afrika ya Kusini uongozi wa shirika hilo uliamua kufanya mageuzi makubwa ikiwemo uingizwaji wa ndege kadhaa mpya na za kukodi katika kuongeza idadi ya ndege zinazotumiwa katika safari za ndani na nje. 

 

Jitihada hizo ambazo ni za kupongezwa hata hivyo zimefikia mahali ambapo wataalamu wa mambo ya usafiri wa anga wanasema kuwa limechochea kuibuka kwa ufisadi wa aina yake ndani ya shirika hilo kongwe nchini.

 

Tarehe 5 Octoba 2007 shirika la ATC liliingia mkataba wa dola milioni 30 wa kukodisha ndege hiyo ya Airbus 320 ambayo wakati mkataba huo unaingiwa ilikuwa nchini El Salvador ikizeeka na kuota kutu. Kabla ya ATC kukubali kuikodisha, ndege hiyo ilikuwa inatumiwa na shirika la ndege la Jamaica ambalo baada ya kuitumia waliiacha katika hali hiyombovu iliyohitaji matengenezo makubwa.

 

Ingawa ndege hiyo imekodiwa na Tanzania kutoka kampuni ya Liberia mkataba wake utaongozwa na sheria za Uingereza. Mdhamini wa ununuzi wa ndege hiyo ni Serikali ya Tanzania ambayo kwa sasa inaongozwa na Chama cha Mapinduzi.

 

Uchunguzi unaonesha kuwa ndege hiyo mbovu ilikuwa El Salvador ikisubiri kuuzwa au kukodishwa kwa mdau mwenye kuja na bei nzuri. Mwanzoni wakati wa kutafuta ndege ya kukodi memo moja ya viongozi wa juu wa ATC ilisema kuwa shirika hilo linahitaji ndege ambayo itakapoletwa nchini “lazima watu wageuze vichwa vyao” kuiangalia inavyoruka.

 

Kwa mujibu wa vyanzo vya habari ndani ya shirika hilo ambavyo kwa sababu wazi vimekataa kutajwa, ndege hiyo ilitakiwa iingizwe nchini Disemba 18 mwaka jana na kuanza safari zake tarehe 21 mwezi huo huo.  A320-214 MSN 630 ndiyo inatarajiwa kufanya safari zake kati ya Dar-es-Salaam na Johannesburg Africa ya kusini.

 

Hata hivyo kutokana na lile sakata la mahujaji na zaidi kutokana na matengenezo makubwa ya kuficha uchakavu wake ndege hiyo imecheleweshwa kuingizwa nchini na sasa inatarajiwa kuingia nchini wakati wowote kuanzia sasa na kuanza safari zake katikati ya mwezi ujao.

 

Ndege hiyo imehitaji kufanyiwa matengenezo makubwa ambayo yamefanyika kwenye hanga ya kampuni ya Aeroman huko huko El Salvador. Mara baada ya ATC kukubali kuingia mkataba huo ukaguzi ulifanyika ili kuangalia hali ya ndege yenyewe ilivyo. Uchunguzi huo ambao ulifanywa kwa kuangalia nje na kutembea ndani ya ndege hiyo.

 

Taarifa ya ukaguzi huo siyo tu ilishtua vigogo wa ATC bali pia ilionesha ni kwa kiasi gani ndege hiyo ilikuwa inahitaji matengenezo makubwa kinyume na mkataba na Wellis Trading Limited ulivyosema. Jambo hilo siyo tu liliwashtua viongozi wa ATC lakini hawakuwa na cha kufanya kwani mkataba ulikuwa umeshaingiwa kati ya ATC na kampuni hiyo yenye makazi yake huko Monrovia, Liberia.

 

Taarifa hiyo ya uchunguzi ilionesha kuwa ndege hiyo ilikuwa na matatizo mengi ambayo yanahitaji matengenezo makubwa. Kwa kuangalia taarifa hiyo kuna mambo hamsini (50) ambayo yanahitaji uangalizi wa karibu na matengenezo ya haraka kabla ya ndege hiyo kuweza kuruhusiwa kuruka.

 

Baadhi ya matatizo hayo ni pamoja na uchakavu wa vitu mbalimbali ambavyo imebidi ATC iingie gharama ya kuvibadilisha kwani mkataba wao na Wellis Trading Inc., unasema wazi kuwa ndege inakodishwa kama “ilivyo” ukiondoa yale mambo ambayo yanasimamiwa na mtengenezaji wa ndege hiyo yaani Airbus au mambo menginee yanayotajwa wazi.

 

Baadhi ya vitu ambavyo vilikuwa na uchakavu mkubwa ni pamoja na vyoo, milango, sehemu ya kuwekea mizigo, mazuria, chumba cha marubani n.k Hata hivyo sehemu kubwa ambayo ilihitaji matengenezo makubwa ni uchakavu usiokifani wa viti vya abiria ambavyo licha ya kuchakaa karibu vyote vilikuwa vimenyofoka nyofoka na vilikuwa vimelegea na kutoa sauti kila mtu anapokalia.

 

Viti vya marubani navyo ni vivyo hivyo huku chumba chenyewe cha marubani kikiwa ni kichafu ambacho mchunguzi mmoja aliyeangalia kwa karibu alisema “viti vyake vinatoa vumbi”. Tatizo la viti kwa kiasi kikubwa limechangia ucheleweshaji wa ndege hiyo hasa kutokana na ukweli kuwa viti hivyo ni maalum na ilihitajika kuweka viti vipya kabisa kwenye ndege hiyo, gharama ambayo mwanzoni ATC haikuwa tayari kuingia wakidai Wallis “haikuwaambia” kuhusu kiasi cha uchakavu huo.

 

Mmoja waliohusika na ukodishaji huu amesema kuwa “Wallis hawakuweka kila kitu wazi kuhusu hali ya ndege”. Hata hivyo haijajulikana kama viti vyote vimebadilishwa na kuwekwa vipya au ndio vimepakwa rangi tu na kufunikwa na vitambaa vipya tu. 

 

Pamoja na hali hiyo chakavu ATC imeshaanza kulipia ndege hiyo na hadi hivi sasa tayari imeshalipia karibu dola milioni moja kwa Wallis na kwa kampuni ya Aeroman (mafundi) na kampuni ya Storm Aviation (wasafirishaji) ambapo marubani na wahandisi wanaoongozana na ndege hiyo wanalipwa na ATC.

 

Mapema mwezi huu ofisi ya Fedha ya ATC iliidhinisha malipo hayo ya mwanzo lakini baadaye ikabidi yasitishwe sababu ya matatizo ya mahujaji. Hadi wiki iliyopita kampuni ya ATC ilikuwa imechelewa kufanya malipo mengine ya dola 370,000 kwa mwezi na hivyo kuadhibiwa faini ya dola 60,000 kwa mwezi.



 
Ni nani anafaa kuingoza Tanzania kama Rais kuanzia 2010-2015?
 

Photo Albums

Just $6.95/Mo
Unlimited Space, Unlimited Transfer, Free Domain
www.bluehost.com

MwanaKijiji.COM LIVE

Window Player   RealAudioPlayer   Itune Player