MwanaKijiji.COM

Wednesday
Mar 10th
Text size
  • Increase font size
  • Default font size
  • Decrease font size
Home arrow NEWS arrow Taifa arrow Mafuriko zaidi? Mwanza na Shinyanga n.k
Mafuriko zaidi? Mwanza na Shinyanga n.k
(1 vote)
Written by M. M. Mwanakijiji   
Saturday, 09 January 2010
ImageKama tulivyotoa taarifa awali ya mafuriko siku ile ya Krismasi, mvua ambazo zimeanza na sehemu nyingine kuendelea kunyesha zimeongeza maeneo ambayo yameathirika na mafuriko na sasa mikoa ya Shinyanga na Mwanza na maeneo ya Mpwapwa na Chamwino huko Dodoma (yakiungana na Kongwa) na eneo ambalo limeathirika zaidi la Kilosa (morogoro) nayo imeanza kukumbwa na athari za mafuriko na kuna uwezekano suala hili likahitaji misaada ya kimataifa na uokoaji.
Hata hivyo, bado kuna sehemu ya mambo ambayo sisi wenyewe kama Watanzania tunaweza kuyafanya na kwa muda sasa kwa kushirikiana na wenzangu walio on the ground tunaandaa one of the biggest relief effort engineered and executed by Tanzanians ever.

Nimezungumza na Katibu Mkuu wa Tanzania Red Cross Mstahiki Meya Alhaji Adam Kimbisa na kuona jinsi gani kwa upande wangu binafsi ningeweza kusaidia na vile vile kwa upande wa wanachama wa mitandao yetu hii na taasisi tunazoshirikiana nazo tungeweza kutoa michango yetu.

Baadaye leo tutakuja na maelekezo ya nini cha kufanya na hasa kwa vile tatizo hili litakuwa la muda mrefu siku tunazoziangalia kwa ajili ya kufikisha misaada hiyo Red Cross ni Alhamisi na Ijumaa ya wiki ijayo (nitaconfirma nanyi).

Kuna ambao nimeaandikia maelekezo kwenye PM wale ambao mmesema mko tayari kushirikiana nami katika kusaidia ndugu zetu waliokumbwa na majanga haya. Ninajua hali ya kiuchumi ni ngumu hasa kwa sisi wengine hapa US na Western Europe na bila ya shaka sehemu nyingine duniani, lakini tunachohitajia si kutoa katika ziada ya utajiri tulionao bali kutoa katika kidogo tulichonacho kuwasaidia wale ambao hata hicho kidogo hawana!

Nakataa kuwaomba wawekezaji waje kutusaidia katika hili; Watanzania tuna uwezo wa kufanya hili kwa kiasi cha utu wetu. Tuamshe ndani yetu ule moyo wa Utanzania wetu na ule uzalendo ambao watu wanadai wanao. Hakuna uzalendo isipokuwa pale unaposimama na taifa lako katika majanga na madhara na kutoa maada wa kila uwezacho.

Kama unafikiri utaweza kusaidia kwa namna yoyote PM ili nikuweke kwenye my next communication; na kama unaweza kuvolunteer muda wako kwa Red Cross naomba uniambie vile vile ili uwe mmoja wa watu wetu pale.

Pamoja tunaweza!
Comments (0)add comment

Write comment

busy
 
Just $6.95/Mo
Unlimited Space, Unlimited Transfer, Free Domain
www.bluehost.com

MwanaKijiji.COM LIVE

Window Player   RealAudioPlayer   Itune Player