MwanaKijiji.COM

Friday
Jul 30th
Text size
  • Increase font size
  • Default font size
  • Decrease font size
Home arrow National arrow Nehemia Mchechu bosi mpya NHC
Nehemia Mchechu bosi mpya NHC
(0 votes)
Written by M. M. Mwanakijiji   
Thursday, 04 March 2010
Breaking NewsWaziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Capt. John Chiligati amemteua Bw. Nehemia Mchechu kuwa Mkurugenzi mpya wa Shirika la Nyumba la Tanzania (NHC). Kabla ya uteuzi huo Bw. Mchechu alikuwa ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Commercial Bank of Afrika. Uteuzi wa Bw. Mchechu umepokelewa kwa fahari na kuridhika na baadhi ya wananchi ambao wanamfahamu kwa karibu Mkurugenzi huyo mpya na zaidi juu ya uwezo wake wa kuonesha uongozi, utendaji na uzalendo. Pamoja na Mkurugenzi mpya shirika hilo pia limepata bodi mpya ambayo itaongozwa na Bw. K. Masudi Issa Msita.

Ifuatayo ni taarifa iliyotolewa na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi juu ya teuzi hizo mbalimbali.

 

Kwa mujibu wa kifungu Na. 18 (1) cha Sheria Na. 2 ya 1990, iliyounda Shirika la Nyumba la Taifa (The National Housing Corporation Act No. 2 of 1990) Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi amemteua Ndugu Nehemia Mchechu (37) kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC). Uteuzi huu unaanzia tarehe 1/3/2010.

Kabla ya uteuzi huu Ndugu Nehemia Mchechu  (pichani) alikuwa Mkurugenzi
Mkuu (Chief Executive Officer) wa Benki ya “Commercial Bank of Africa”.

Chini ya Uongozi wake benki hiyo imepata mafanikio makubwa sana hapa nchini, na ni moja kati ya benki tano zilizoanza utaratibu wa kutoa mikopo ya nyumba kwa Watanzania.


Ndugu Nehemia Mchechu akishirikiana na Bodi mpya ya Shirika hili na timu ya Menejimenti ya Shirika hili, amepewa jukumu la kulifanyia mageuzi makubwa Shirika hili ili liingie katika biashara kubwa ya kujenga nyumba katika Mikoa yote na kuziuza kwa mikopo kwa watanzania wa kipato cha chini na kati, ambalo ndilo lengo kuu la Shirika hili tangu lilipoanzishwa mara tu baada ya Tanganyika kupata Uhuru Desemba 9, 1961.

Wakati huo huo, na kwa mujibu wa Sheria Na. 2 ya 1990 iliyounda Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amemteua Bwana K. Masudi Issa Msita kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika hilo. Bwana K. Masudi Issa Msita ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Ujenzi (National Construction Council).

Wakati huo huo, na kwa mujibu wa Sheria hiyo hiyo, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi amewateua wafuatao kuwa Wajumbe wa Bodi ya Shirika hilo.
1. Msajili wa Hazina - (Wizara ya Fedha).
2. Mkurugenzi wa Nyumba - (Wizara ya Ardhi).
3. Prof. W.J. Kombe - (Chuo Kikuu cha Ardhi).
4. Bwana Enock Maganga - (Benki Kuu).
5. Bi Subira Mchumo - (Sekta Binafsi).
6. Bwana Elius Mwakalinga - (Wizara ya Miundombinu).
7. Bi. Shally Raymond - (Mbunge)
Uteuzi huu unaanza tarehe 28/02/2010 na ni wa miaka mitatu.


Imetolewa na:-
Wizara ya Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi

Comments (0)add comment

Write comment

busy
Last Updated ( Thursday, 04 March 2010 )
 
Just $6.95/Mo
Unlimited Space, Unlimited Transfer, Free Domain
www.bluehost.com

MwanaKijiji.COM LIVE

Window Player   RealAudioPlayer   Itune Player