|
Prof. Jwani Mwaikusa, 2 wauawa! |
|
Written by M. M. Mwanakijiji
|
|
Wednesday, 14 July 2010 |
Habari ambazo zimeingia sasa hivi ni kuwa Prof. Jwani Mwaikusa ameuawa. Pamoja naye taarifa zinadokeza kuwa mwanae pia ameuawa. Tunaendelea kufuatilia taarifa hizo kwa karibu ili kuweza kupata taarifa za uhakika zaidi. Wengi tunamfahamu hivi karibuni katika kesi ya wagombea binafsi akiwa mmoja wa walioitwa kuwa "marafiki wa mahakama" yeye akitetea haki ya wagombea binafsi na kusisitiza kuwa mahakama ina uwezo wa kusikiliza kesi hiyo.
Taarifa zinadokeza kuwa mauaji hayo yametokea nyumbani kwake usiku wa kuamkia leo. Taarifa bado zina kiza kuna uwezekano wa zaidi ya watu wawili kuwa wameuawa kwenye tukio hilo..
|
|
Last Updated ( Wednesday, 14 July 2010 )
|