MwanaKijiji.COM

Monday
May 21st
Text size
  • Increase font size
  • Default font size
  • Decrease font size
Home arrow National arrow Taifa arrow Wanaoua Albino nao wauawe - Pinda
Wanaoua Albino nao wauawe - Pinda
(0 votes)
Written by Mwananchi   
Friday, 23 January 2009

Albino KATIKA hali ya isiyo ya kawaida, Waziri Mkuu Mizengo Pinda jana aliwaambia wananchi kuwa wanaoua watu wenye ulemavu wa ngozi (albino) pamoja vikongwe ni hawana budi kuuawa kwa kuwa wakisubiri mahakama kuwahukumu, watakuwa wanakosea. Waziri Pinda, ambaye ameanza ziara katika mikoa ya Kanda ya Ziwa yenye lengo la kuhamasisha vita dhidi ya mauaji ya vikongwe na albino, aliutaka Umoja wa Vijana wa CCM kuongoza vita hiyo, akisema lina jeshi zuri.

Mauaji ya albino yamekuwa ni tatizo kubwa nchini na hasa katika mikoa ya Kanda ya Ziwa.

Pamoja na serikali kutangaza hatua kadhaa za kupambana na wauaji hao, bado matukio ya kuuawa kwa watu hao wenye ulemavu wa ngozi yamekuwa yakiendelea kuripotiwa, lakini Waziri Pinda ameenda mbali zaidi katika kukabiliana na tatizo hilo alipotaka wauaji hao wauawe badala ya kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria.

Kauli ya Pinda, ambayo inaweka maswali katika suala la utawala bora, imekuja wakati ambao wananchi wamekuwa wakijichukulia sheria mkononi na kuua vikongwe kutokana na imani za uchawi.

Akihutubia wakati wa kufungua mkutano wa 16 wa Shirikisho la Vyama vya Kuweka na Kukopa (SCCULT) kwenye ukumbi wa Chuo cha Utumishi Umma mkoani hapa, Waziri Pinda alisema iwapo wananchi wataendelea kuwahurumia wauaji hao ambao wanatafuta viungo vya albino wakitegemea mahakama itatenda haki huku nao wakiongeza kasi ya mauaji kwa Watanzania, watakuwa wanakosea.

Hivyo alisema kwamba kuanzia sasa mtu yeyote atakayemuona mtu amemkata shingo au mkono mweziwe basi naye auawe papo hapo hii itakuwa ndiyo dawa kwani vingozi wote tumechoka na mauji hayo.

"Mkimuona mtu akamkata mwingine shingo naye muueni kwani sasa viongozi wote tumechoka... no more, I can't tolerate anymore (imetosha, siwezi kuvumilia tena)," alisema Pinda huku akiwaacha watu midomo wazi.

Aliviomba vyama vya siasa kushirikiana na wananchi kuhakikisha suala hili la mauji linakwisha kwani wauji "tunaishi nao na ni rahisi kulimaliza iwapo tutakuwa kitu kimoja katika kuondoa kashifa hii ambayo imekuwa mbaya kwa nchi yetu".

Aliuagiza Umoja wa Vijana wa CCM kuhakikisha mauaji hayo yanatokomezwa kabisa, akisema kuwa ni jeshi zuri ambalo likiamua kutokomeza kabisa mauaji ya vikongwe na ndugu zetu maalbino inawezekana.

"Umoja wa vijana mna jeshi zuri ambalo naamini mkiamua mnaweza kutokomeza mauaji ya wazee wetu pmoja na ndugu zetu maalbno na kazi hiyo nawaagiza muanze leo msisubri auawe mwingine tena," alisema waziri mkuu.

Baada ya kumalizika kwa mkutano huo, baadhi ya watu wanaoonekana kuwa ni wa "serikali" waliwafuata baadhi ya waandishi wa habari, akisihi suala hilo lisiripotiwe magazetini kwa madai kuwa kauli hiyo ya Waziri Pinda inaweza kusababisha matatizo.

Rais Jakaya Kikwete, ambaye pia amekuwa mstari wa mbele kupiga vita mauaji hayo, alitofautiana na Waziri Pinda katika moja ya hotuba zake aliposema kuwa adhabu ya kuua haitofautishi muuaji wa albino na muuaji mwingine na kwamba watakaopatikana na hatia ya kuua albino, atakabiliana na adhabu ya kifo kama ilivyo kwa muuaji mwingine.

Waziri Pinda alionekana kukerwa na mauaji ya albino wakati alipopata taarifa kwamba kuna mama mwingine aliuawa usiku wa kuamkia juzi.

"Nimeambiwa kuwa juzi wilayani Sengerema kuna mama mmoja ambaye ni mlemavu wa ngozi amekatwa mkono na wauaji wakaondoka na mkono huo na tayari mama huyo amekufa," alisema Pinda na kusisitiza kushughulikia wauaji hao.

Akitoa takwimu za mauaji ya vikongwe na malbino alisema mwaka 2003 waliuwawa vikongwe 517, mwaka 2004 waliuawa vikongwe 444, mwaka 2005 (494), 2006 (vikongwe 386), mwaka 2007 (vikongwe 526) na albino sita na mwaka 2008 (vikongwe 526 na albino 28).

Alisema tayari mwaka huu wameuawa albino watatu hivyo kufanya albino na vikongwe waliouawa kufikia kuwa jumla 2,900.

Waziri mkuu ameanza ziara ya siku nne kutembelea mikoa ya Shinyanga, Tabora na Mwanza ili kuhamasisha wananchi watokomeze vitendo vya mauaji ya vikongwe na watu weye ulemavu wa ngozi.

Comments (6)add comment
kijana: ...
pinda hapo umeongea,hakuna cha kupelekana mahakamani kwa watu wa aina hiyo,ni kuwakata vipande vipande tu bila huruma
1

January 24, 2009
Votes: +1
Kungulilo: ...
Hili ni eneo jingine ambalo serikali imeonyesha kushindwa katika utendaji wake na kudhibiti na sasa tunakuja na mtindo wetu wa "zima moto" maana hakuna hata eneo moja ambalo tuliowapa dhamana wanawajibika kwa usahihi,maneno meeeeengi lakini utendaji hakuna!
2

January 24, 2009
Votes: +0
Japhet B. Kanizius: ...
Kweli suala la mauaji ya yanasikitisha sana. Pia yametutia aibu kubwa sana. Maziri kama binadamu mwingine naona aliongelea jambo akiwa ametawaliwa na uchungu mkubwa sana. Lakini mbali na kuhuzunishwa huko, amekosea kuawaagiza wananchi wajichukulie sheria mkononi. Tanzania ni nchi iliyofikia mafanikio makubwa sana katika utekelezaji utawala wa sheria Barani Afrika. Hivyo, haiwezekani wananchi kujichukulia sheria mikononi. Nadhani angetumia uchungu aliokuwa nao kuwaomba wanaanchi wawataje wahusika kwani baadhi ni ndugu zao, waume zao na hivyo wanawafahamu. Mbali na nguvu ya vyombo vya dola inayoendelea kutumika kuwasaka makatili hao, lakini pia kuna umuhimu wa kuongeza juhudi katika kuwaelimisha na kuwahamasisha wananchi washirikiane na serikali katika ulinzi shirikishi ambapo kazi yao ni kuhakikisha wanawaanika watu wenye nia mbaya na nchi yetu ambao wanakaa miongani mwa jamii. Pia, waganga wa jadi waelimishwe nao waone kwamba wanachokifanya si kizuri. Walengwa wote wakielimishwa itakuwa ni mchango mkubwa kwa jitihada za nguvu ya dola za kukomesha ukatili huu.

Japhet Kanizius
Netherlands
3

January 24, 2009
Votes: +0
ben: ...
NIMESHITUSHWA SANA NA MATAMSHI HAYA YA KIONGOZI WA TAIFA ALIYESOMEA SHERIA - ANAWAFUNDISHA WANANCHI KUCHUKUA SHERIA MIKONONI MWAO!! - PAMOJA NA HASIRA ZOTE TULIZO NAZO BADO KUNA VYOMBO VYA SHERIA NA UTAWALA WA SHERIA -KAMA VIMESHINDIKANA BASI PINDA ATUELEZE HIVYO BADALA YA HII POPULIST POLITICS - KUNA USEMI KUWA UKIVUNJA SHERIA NAYO ITAKUVUNJA - IKO SIKU MTINDO HUU WA MOB JUSTICE UTATUMEZA SIYE WENYEWE - MHE. PINDA SAHIHISHA USEMI WAKO - MHE RAIS SEMA NAYE AJISAHIHISHE KAMA AMETELEZA - NASHANGAA WANAHARAKATI NA WANASHERIA NA MAJAJI WAMENYAMAZA KIMYA - MWAMBIENI PINDA "HAPO UMEKOSEA"
4

January 27, 2009
Votes: +0
Benard: ...
Pinda amekosea. Aombe radhi kwa Watanzania mara moja. Ni hatari sana kwa kiongozi wa kitaifa kuhamasisha wananchi wajichukulie hatua mkononi. Utawala wa sheria uko wapi??? Mahakama na polisi kazi zao ni zipi sasa???
Pinda futa usemi wako mara moja....jisafishe uso kwa kutoa kibanzi
5

January 27, 2009
Votes: +0
Nelson N Mwambala: ...
Suala la mauaji LINASIKITISHA SANA. Pia limetutia aibu kubwa sana ulimwenguni. MIMI NINAMUUNGA MKONO WAZIRI MKUU KWA ASILIMIA ZOTE. Haya mambo kama utawala wa sheria uliotupatia sifa na mauaji ya albino ni vitu viwili visivyoendana. Tukumbuke kuwa aibu tunayoipata ulimwenguni pote duniani ni kubwa mno kiasi kwamba inafunika sifa hizo wajumbe wanazozingumzia.
Na tukizingatia kiubinadamu nina imani kuwa maneno hayo ni yakujifurahisha tu ili watu wengine wawaone kuwa wanafahamu sana mambo ya sheria. Lakini uhalisia wake ni kwamba watu kama hawa bila shaka hawana ndugu (albino) ambao wamewahi kukumbwa na hali hii na hivyo hawana uchungu hata kidogo na ndugu zetu - maalbino.
Jambo hili halina tofauti sana na lile la wauaji kuhukumiwa kifo. Wanaharakati wanataka kutuambia kuwa wauaji wana haki ya kusikilizwa na kuishi kuliko maalbino! Hii haiwezi kuvumiliwa hata kidogo!
Hivi hawa watu walitaka waziri Pinda awambie nini wananchi - si yangekuwa yaleyale? Kadiri kesi zinavyovidi kuchelea ndivyo wauaji wanavyoamini kuwa kuwepo kwa adhabu ya kifo kwao itategemea na jinsi watakavyojieleza kwenye kesi.
Hivi angekuwa mtoto wako unamkuta anachinjwa laivu ungesubiri hadi huyo mtu afikishwe mahakamani? Kibinadamu hakika mimi ningekosa uvumilivu! Na nina imani Pinda alikuwa anajaribu kulimaliza tatizo kwa kuwa anaamini kuwa watu hawa hawaelimiki hata ukijitahidi namna gani. Watanzania tulio wengi si tu kwamba hatuna utamaduni wa kujisomea bali pia hata wa kusikiliza redio, au kuangalia video. Na hata unapowakuta wanasoma au wanasikiliza redio au kuangalia video yanakuwa ni mambo ya michezo tu.
Kingine ni kwamba watanzania wengi hawaogopi kufikishwa mahakani kwa vile wanajua kuwa kule ndiko usalama wao uliko. Wengi wao ni mpaka waone adhabu inatekelezwa ndipo watakapoogopa, na ndipo heshima ya taifa itakaporejea.
Kama tunaogopa machafuko mbona vibaka/wezi wanauliwa na wale wanadhaniwa kuwa ni wananchi wenye hasira kali na bado watu wanaendela kuishi kwa kueshimiana na amani. Mbona machafuko hayaendelei?
Ni kweli kuwa tuna Katiba lakini wakati fulani ili kukabiana na mambo fulani yaliokithiri hatuna budi tuende na hali halisi kwanza na kwa vitendo, ili kumnusuru binadamu kwanza mwenye hadhi na haki sawa na sisi na kwa maslahi ya Watanzania wote. Si nyakati zote kwamba katiba itakuwa 'applicable', na wala si jambo la kisiasa ila ni jambo la utu. Na wakati mwingine ni vizuri zaidi kumpa nafasi kiongozi kama huyo kuchukua uamuzi mwafaka kulingana na hali halisi haswa katika maswa la nyeti kama hayo.
'After all' jambo hili ni la dharula na kama sisi kweli ni binadamu tunaojali utu ni lazima tutachukua hatua ya haraka. Ni lazima twende na wakati na tuchane na mambo ya kukariri katiba inasema nini hata kama ufumbumbuzi utakaopatikana hautaendana na hali halisi. Watu wengine watatumia mwanya huo kuponea.

Nelson NM
6

January 29, 2009
Votes: +0

Write comment

busy
Last Updated ( Tuesday, 27 January 2009 )
 
Ni nani anafaa kuingoza Tanzania kama Rais kuanzia 2010-2015?
 

Photo Albums

Just $6.95/Mo
Unlimited Space, Unlimited Transfer, Free Domain
www.bluehost.com

MwanaKijiji.COM LIVE

Window Player   RealAudioPlayer   Itune Player