Rais Kikwete amesema kuwa serikali yake imekubali kimsingi hoja ya kuangalia Katiba yetu ili hatimaye tuweze kuwa na Katiba inayokidhi mahitaji yetu. Rais Kikwete amesema hayo katika salamu zake za Mwaka mpya leo Ijumaa. Kukubali kwa Rais Kikwete na serikali yake ni jaribio la kuepusha mgongano ambao ulikuwa unakuja mbele ambapo vyama vya siasa na wananchi wamekuwa wakipaza sauti kutaka Katiba yao iangaliwe upya na hata kuwa na Katiba Mpya. Hata hivyo, Rais hajaweka muda maalum wa kumaliza mchakato huo ambao ameuahidi kuanza mara moja na badala yake ameacha jukumu hilo kwa Tume ya Kupitia Kati...