MwanaKijiji.COM

Wednesday
Feb 08th
Text size
  • Increase font size
  • Default font size
  • Decrease font size
Home arrow Siasa arrow Siasa arrow CCM na Rushwa, hatimaye kuku wamerudi kutamia!
CCM na Rushwa, hatimaye kuku wamerudi kutamia!
(0 votes)
Written by M. M. Mwanakijiji   
Thursday, 29 July 2010
ImageTumepiga kelele kwa miaka minne na kelele zetu zimebatizwa kuwa ni "chuki binafsi". Tumewapigia mbiu waamke lakini panda zetu zimekuwa ni "kelele za mlango" ambazo hazimzuii mwenye nyumba kulala. Tumesema mfumo wa utawala wa kifisadi nchini ni matokeo ya utawala wa CCM, wakatuambia kuwa 'ufisadi ni wa mtu mmoja mmoja na siyo chama". Wengine wakathubutu kutuambia kabisa kuwa "mafisadi ndani ya CCM ni wanne na wamefikishwa mahakamani". Tumesema ufisadi ni matunda na mazao ya utawala wa CCM na watu wengine wanasema tumefanya hivyo kwa sababu tuna "wivu". Sasa twayaona matunda ya ufisadi uliokithiri na mfumo wenye kulea ufisadi. Leo tunashuhudia jinsi vyombo vya kusimamia sheria (law enforcement agencies) vikicheza kama "ukuti ukuti" na vitendo vya rushwa huku wakituonesha mazingaombwe ya kuwa wako makini.

Matukio mbalimbali nchi nzima ambapo mchakato wa kutafuta nafasi ya kugombea ndani ya CCM umegubikwa na vitendo vya rushwa na ufisadi. Hii yote si kitu kingine bali ni AIBU YA CCM. Leo hii tunaweza kujua kabisa kile alichouliza Mwalimu kina mantiki kubwa sana. Kwamba hawa wanaotumia fedha nyingi kutaka kuingia madarakani tena kwa njia za giza giza watarudisha vipi fedha zao hizo wakiingia madarakani?

Ukweli ni kuwa siri ambayo inajulikana kwa muda mrefu sasa inawakodolea CCM machoni kama jogoo linalosubiri kuchinjwa, yale ambayo yalikuwa yanafanyika kwa kificho sasa yanakuja hadharani. Matokeo yake PCCB, TISS, POlisi na Mwanasheria Mkuu wote wanajikuta hawana ujanja wa cha kufanya.

Hawawezi kuwatia pingu wote bila kuharibu mchakato wa uchaguzi wa CCM; hawaweti kuwasimamisha wote kugombea kwa sababu kwa kufanya hivyo "nani msafi" atakayeshika madaraka. Kumbe siri ya uchafu wa CCM ni kubwa zaidi.

Hii ni aibu ya CCM na aibu ya wale wote ambao wamejipanga kuishangilia. Haiwezekani kuwa na mtindo mbovu wa kuingia madarakani ambao ungezaa mtindo mzuri wa utawala wakiwa madarakani. Kama hawa watu wanajihusisha na vitendo vya kifisadi kabla ya kuingia madarakani itakuwaje watakaposhika madaraka? Kama leo wanajaribu kuuharibiana na kuumizana kabla hawajakutana na wapinzani Augusti 20 itakuwaje baada ya hapo?

Tunachoshudia basi ni maandalizi ya vitenvo vibaya kabisa vya uchaguzi mkuu tutakavyoviona. Kama ambavyo imedokezwa na mtu mwingine kuwa hadi tarehe moja hakuna mwana CCM ambaye anadaiwa kuwa amejihusisha na vitendo vya rushwa atakayefishwa mahakamani. HAKUNA. Wote ambao wanadaiwa "kukamatwa" watashiriki kana kwamba hawana tuhuma.

Ninaamini, kwenda kuwaengua wagombea hao kwenye vikao kwa kutumia ushahidi wa "TAKUKURU" itakuwa ni kitendo cha kiwoga zaidi. CCM isikimbie utawala wa sheria. Kama TAKUKURU ina kesi dhidi ya watu hao basi wasiruhusiwe kushiriki kura za maoni kabisa na waondolewe kabla ya majina yao wagombea kutangazwa na Kamati Kuu Augusti 14.

Tunachoshuhudia ni kile kile ambacho tunakijua kuwa "kile unachopanda ndicho unachovuna". Kwa muda mrefu CCM imepanda mbegu za ufisadi ndani ya wanachama wake na uongozi wake, na sasa wanavuna matunda yake na nina uhakika watavuna zaidi mavuno haya ya ufisadi kuelekea uchaguzi mkuu. Hatimaye kuku walioenda mitaani kucheza na majogoo ya ufisadi, sasa wamerudi CCM kutamia.

CCM itaelea vifaranga.
Comments (1)add comment
Eddie: ...
Kwanza napenda kukupongeza kwa article yako ambayo nathubutu kukwambia kuwa umeiandaa kwa jicho linalostahili hasa! Hv kwa mtizamo wa nje wa matendo ya rushwa yanayoeendelea hasa kTk kipindi hiki cha michakato ya kuwapata wagombe wa hicho kinachoitwa chama tawala kuelekea uchaguzi mkuu tunapata nn! Hv n format kwamba viongozi ni lzm wawe wakina fulani huku watanzania wakipiga makofi kufurahia ujinga ambao utawaumiza baadaye! kweli imefikia watanzania tunakubali kudanganyika kirahisi namna hiyo halafu nn matokeo yake! Kwa wale wanaofanya vitendo vya rushwa huku takukuru wenye nafasi ya kuzuia kwa makisudi wanakurupuka huku wakiharibu ushahidi tunataka tuwe na viongozi wa namna gani! Watajali kweli maslahi ya watanzania walio wengi!wkt mwingine nasikikia kichefuchefu nikianza fikiria chaguzi za nchi ya dunia ya tatu hususan Tanzania. Natamani wote tungekuwa na jicho kama ulilonalo na tukalitizama hili kwa mlengo mwingine!
1

August 01, 2010
Votes: +1

Write comment

busy
 
Ni nani anafaa kuingoza Tanzania kama Rais kuanzia 2010-2015?
 

Photo Albums

Just $6.95/Mo
Unlimited Space, Unlimited Transfer, Free Domain
www.bluehost.com

MwanaKijiji.COM LIVE

Window Player   RealAudioPlayer   Itune Player