MwanaKijiji.COM

Monday
May 21st
Text size
  • Increase font size
  • Default font size
  • Decrease font size
Home arrow Siasa arrow Siasa arrow CCM yaomba radhii kwa kuingiza Udini uchaguzi mkuu
CCM yaomba radhii kwa kuingiza Udini uchaguzi mkuu
(0 votes)
Written by Habari Leo   
Tuesday, 04 January 2011
ImageKATIKA kuonesha uungwana na ukomavu wa kisiasa, Waziri Mkuu Mizengo Pinda kwa niaba ya CCM na Serikali yake, amewaomba radhi viongozi wa dini nchini kutokana na kauli kinzani zilizotolewa na baadhi ya wagombea wa chama hicho mwaka jana.  Wagombea hao katika uchaguzi wa mwaka jana, walitoa kauli mbalimbali zilizokinzana na imani za dini zao. Pinda aliwaomba radhi viongozi hao wa dini nchini kote jana kupitia kikao cha pamoja chake, viongozi hao na baadhi ya wazee maarufu wa hapa kilichofanyika kwenye ukumbi wa Libori.

Alisema uchaguzi mkuu uliopita haukuwa laini kama ilivyotarajiwa … ulikuwa na changamoto nyingi zikiwamo tofauti za kimtazamo na kiimani, hivyo kwa yaliyojitokeza ya baadhi ya wagombea kugusa imani za dini za watu, halikuwa lengo lao kufanya hivyo na “tunaomba mtusamehe kwa yote yaliyojitokeza na kukwaza imani za dini zenu.

"Hali hiyo si kwamba ilijitokeza tu Sumbawanga ... najua tulimkwaza Mhashamu Baba Askofu (Damian Kyaruzi), tulikejeli imani ya dini yake, tunaomba radhi, mimi naomba radhi kwa
niaba ya CCM na Serikali.

“Si hapa tu lakini ni maeneo mengi nchini kama vile majimbo ya uchaguzi ya Hai na Same, ambako baadhi ya wagombea katika kuomba kura ya ndiyo walilazimika kutumia baadhi ya maneno yanayotumika katika Injili ya Mateso," alisisitiza Waziri Mkuu.

Alisema kutokana na hali iliyojitokeza CCM na Serikali wamepata fundisho, na katika uchaguzi ujao, aliomba viongozi wa dini, Serikali na vyama vya siasa, wakae pamoja kuweka angalizo ili wagombea wajiepushe na kejeli dhidi ya imani za dini za wengine na kuwasihi viongozi hao nchini kuanza ukurasa mpya na kutumia muda mwingi kuhamasisha maendeleo.

Akizungumzia rushwa, alikiri kukithiri katika uchaguzi mkuu huo na kuongeza kuwa ipo haja ya kuangalia upya mfumo wa uchaguzi kuanzia ndani ya CCM ambayo inajiandaa kwa uchaguzi wa viongozi wake mwakani kuhakikisha haitoi mianya ya rushwa na viongozi wa dini na wazee wakemee kwa nguvu zote rushwa.

"Rushwa ni rushwa tu, hakuna haja ya kusema kuna ndogo, hata mtu anapotaka kutimiza haja zake fulani kwa kutoa kitu kidogo ni rushwa ... pia kwa mgombea anapotoa doti ya khanga ili apigiwe kura, ni tatizo hivyo naiomba CCM ibadilike, najua ni jambo gumu lakini lazima tupigane nalo kikamilifu ... wagombea nao tabu tu, hasa kwenye chama safari hii tujirekebishe," aliasa.

Akishukuru, Mwenyekiti wa Umoja wa Makanisa ya Kikristo Tanzania Mkoa wa Rukwa, Mchungaji Israel Moshi, alisema madhebu ya dini yamesamehe, na viongozi wanapaswa kusamehewa, kwani wote ni binadamu na wanapaswa kusameheana kwa ajili ya maendeleo ya Rukwa na Taifa kwa jumla.

Akitoa mchango wake, Mhashamu Baba Askofu wa Anglikana Jimbo la Sumbawanga,
Marco Badeleya, alizungumzia Katiba mpya na kumpongeza Rais Jakaya Kikwete kwa kusikia kilio cha Watanzania juu ya kupata Katiba hiyo lakini akashauri kamati itakayoratibu upatikanaji wa Katiba hiyo, iundwe na watu waadilifu itakayoridhisha na kukidhi matarajio ya Watanzania.

Baadhi ya wachunguzi wa masuala ya siasa wameipongeza hatua ya Pinda kuwa muwazi na kukubali udhaifu kwa kuomba radhi na kusema hiyo ni njia ya kujenga utangamano katika jamii lakini pia kutambua mtu alikojikwaa na kujirekebisha.

 

Maoni Yetu:

Hatua ya pili ni kwenda kuwaomba radhi jamii ya Waislamu nayo. 

Comments (2)add comment
selemani ally adam: ...
Nijambo la busara sana alilolifanya mheshimiwa waziri mkuu la kuomba radhi viongozi wa dini.Kwani hakuna kitu hatari katika nchi kupoteza amani kama udini,na sisi hatuna asili hiyo,ya serikali yende kiserikali.
1

January 12, 2011
Votes: +2
Tumbo: ...
Pm! huo ni unyenyekevu wako binafsi Mungu akupe maisha marefu !!!! mtu mzima umkweli na muungwana baba mwema, kaka mpole, ndugu mwenye hekima!!
2

October 01, 2011
Votes: +1

Write comment

busy
Last Updated ( Tuesday, 04 January 2011 )
 
Ni nani anafaa kuingoza Tanzania kama Rais kuanzia 2010-2015?
 

Photo Albums

Just $6.95/Mo
Unlimited Space, Unlimited Transfer, Free Domain
www.bluehost.com

MwanaKijiji.COM LIVE

Window Player   RealAudioPlayer   Itune Player