|
Dr. Slaa mgombea Urais wa Chadema 2010 |
|
Written by M. M. Mwanakijiji
|
|
Tuesday, 20 July 2010 |
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA0) Dr. Wilbroad Slaa amependekezwa kuwa Mgombea wa chama hicho kwa Kiti ch a Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Uamuzi wa kuingia kwenye kinyang'anyiro cha Urais kwa Dr. Slaa unabadili kabisa mwelekeo wa upepo wa usindi wa CCM ambao hadi sasa ulikuwa unanukia kuwa utakuwa ni wa kishindo. Dr. Slaa ambaye amekuwa mbunge wa chama chake kutokea Karatu kwa miaka 15 sasa anaingia ulingoni akipambana na Rais Kikwete ambaye naye amepitishwa hivi karibuni kuwa mgombea wa chama chake. KLHN bado inasubiri kupata taarifa za nani atampendekeza kuwa mgombea mwenza wake.
|