Rais Kikwete ameikana rasmi kampuni ya Dowans (japo hakusema ni Dowans ipi) akitamka kwa mara ya kwanza hadharani kuwa hana maslahi ya aina yoyote katika kampuni hiyo. Rais Kikwete ameyasema hayo akiwahutubia mamia ya wanachama na mashabiki wa CCM kwenye maadhimisho ya miaka 34 ya Chama cha Mapinduzi yaliyofanyika mjini Dodoma siku ya Jumamosi. Akigusia suala la malipo ya bilioni 94 ambayo Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi iliiamua kampuni ya Dowans ilipwe na Tanesco Rais Kikwete amesema kuwa serikali yake itafanya kila njia za kisheria ili kampuni hiyo isilipwe.
watawala wote afrika wasipoangaliwa kwa karibu na watawaliwa wao ( raia) wanamuelekeo mmoja wa kuelekea ufisadi,kujinufaisha,kufuja fedha na matumizi mabaya ya madaraka.