|
Meya Kimbisa kupokea misaada ya wahanga wa mafuriko |
|
Written by M. M. Mwanakijiji
|
|
Friday, 15 January 2010 |
Misaada yetu ya kwanza tuliyokusanya siku hizi mbili itakabidhiwa kesho leo Ijumaa Kwa Katibu Mkuu wa Chama cha Msalaba Mwekundu cha Tanzania ambaye pia ni Meya wa Jiji la Dar-es-Salaam Mstahiki Alhaji Adam Kimbisa majira ya saa kumi hivi (kama muda haujabadilika). Misaada hiyo ni pamoja na vitu mbalimbali vya mahitaji ya kutosheleza familia kadhaa pamoja na fedha taslimu zilizochangwa na Watanzania sehemu mbalimbali duniani.
Tunatumaini hii itakuwa ni hamasa ya kuwahakikishia watanzania wenzetu kwamba katika hili tuko makini na tunataka kuonesha kuwa tunaweza. Taarifa ambazo bado zinaingia zinaonesha hali bado haijatulia hasa huko Kilosa kwani mto unazidi kufurika na watu wengi zaidi wanazidi kuathirika na hivyo misaada yetu inahitajika zaidi leo hii. Kwa wale walioko Marekani unaweza kuchangia kupitia Paypal ya mtandao wa mwanakijiji.com (fedha zilizochangwa siku hizi mbili, tayari zimeshatumwa Tanzania ziunganishwe na misaada mingine). Kwenye mtandao huo unaweza kutumia kadi za Kibenki kwa njia salama kabisa (secure transaction). Nasikia mmojawapo wa mawaziri atakuwepo kuwasilisha michango yetu hii kwa Red Cross akionesha mshikamano na umoja. Wale ambao bado wanasubiri sijaelewa wanasubiri nini hasa.. join now; be part of change, don't wait for change to happen, you'll wait unchanged! Taarifa zaidi baadaye: Kama uko Tanzania .. unaweza kuchangia waathirika wa mafuriko wa Tanzania: Text "TPN" kwenda namba 15522. Utakatwa Shs 250 kujisajili. Na utachangia Shs 150.00 kwa siku thelathini; sawa na 4500Ths! Hii ni sawa na kuchangia dola 3.46 kwa mwezi!! Kama uko nje ya nchi unaweza kutumia mtandao wetu hapa upande wa kulia ukurasa wa mbele au upande wa juu kwenye Forum kuna kitufye kinachosema "Donate" na unaweza kutumia kadi zozote za kibenki katika njia salama ambayo tumeshaitumia mara kadhaa katika michango mbalimbali. the amount raised will be contributed to the Tanzanian Red Cross Society
|