|
Shein mgombea Urais wa CCM Zanzibar |
|
Written by Michuzi na M.M. Mwanakijiji
|
|
Friday, 09 July 2010 |
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Mohammed Shein amependekezwa na Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM kuwa mgombea wa kitu cha Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya chama cha mapinduzi. Akiwatupilia mbali wagombea wengine 11 Dr. Shein ambaye adhma yake ya kugombea Zanzibar imetengezwa wiki chache tu zilizopita mwelekeo wa siasa za Zanzibar sasa unaonekana kuwa mgumo zaidi kuliko ilivyokuwa inatarajiwa hasa kukiwa na kundi la watu ambao wanaamini Dr. Shein si mwanasiasa anayeweza kushindana na chama cha Upinzani visiwani mle. Hata hivyo maoni ya wachunguzi wa kisiasa yanadokeza kuwa yote yatategemea sana mwitikio wa Dr. Ghaib Bilal ambaye alipata kura za 54 na Nahodha Vuai ambaye alipata kura 33 dhidi ya kura 111 za Dr. Shein.
Siku ya Jumapili mgombea wa CCM kwa kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Rais Kikwete anatarajiwa kutangaza mgombea mwenza wake ambapo hatimaye timu nzima ya nafasi za juu za kisiasa nchini kwa upande wa CCM zitakuwa zinajulikana huku mchakato wa nafasi za ubunge kuanza kuwiva mara tu baada ya Bunge hili kuvunjwa Ijumaa wiki ijayo. Aliyekuwa Rais wa Zanzibar kwa kipindi cha miaka kumi iliyopita Bw. Karume anatarajiwa na wachunguzi wengi kutangazwa kuwa mgombea mwenza pamoja na Rais Kikwete. Hata hivyo majinga mengine ambayo yametajwa ni pamoja na Dr. Salim na Zakhia Meghji aliyewahi kuwa Waziri wa Fedha chini ya Rais Kikwete. Mgombea urais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi Dr.Ali Mohamed Shein akiwashukuru wajumbe wa Halmashauri kuu ya taifa CCM kwa kumchagua kuwa mgombea urais kwa tiketi ya CCM usiku wa kuamkia leo mjini Dodoma.
Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza makamu wa Rais Dr.Ali Mohamed Shein kwa kuchaguliwa na wajumbe wa Halmashauri kuu ya Taifa CCM kuwa mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi katika ukumbi wa White house mjini Dodoma usiku wa kuamkia leo. Mwenyekiti wa CCM ,Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongoza kikao maalumu cha Halmashauri kuu ya taifa CCM kilichompitisha Dr.Ali Mohamed Shein kuwa mgombea wa Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza Dr.Gharib Bilal kwa kukubali matokeo ya ushindi wa Dr.Ali Mohamed Shein kuwania urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM Mwanasiasa Mkongwe Kingunge Ngombale Mwiru akimpongeza Dr.Gharib Bilal kwa kukubali matokeo ya uchaguzi ambapo Dr.Ali Mohamed Shein aliibuka mshindi katika ugombea urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM mjini Dodoma. Dr.Mohamed Gharib Bilal akimpongeza Dr.Ali Mohamed Mohamed shei kuchaguliwa mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM mjini Dodoma. Baadhi ya wajumbe wa halmashauri kuu ya Taifa CCM wakiwa katika kikao maalum kilichompitisha Dr.Ali Mohamed Shein kuwa mgombea wa urais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi usiku wa kuamkia leo mjini Dodoma
|
|
Last Updated ( Saturday, 10 July 2010 )
|