MwanaKijiji.COM

Wednesday
Feb 08th
Text size
  • Increase font size
  • Default font size
  • Decrease font size
Home arrow Siasa arrow Siasa arrow Sitta jemedari aliyesalimu amri?
Sitta jemedari aliyesalimu amri?
(6 votes)
Written by M. M. Mwanakijiji   
Tuesday, 18 August 2009
ccmlogoHabari ambazo zimekuwa zikitiririka kwa muda wa masaa kadhaa yaliyopita zinatuthibitishia kuwa waoga wanaongoza CCM sasa hivi. Habari za kuwa Spika wa Bunge la Muungano alipewa kibano katika mojawapo ya vikao vya juu vya CCM ni habari za kuudhi, kukera, na kuchekesha; yote kwa kwa wakati mmoja. Vile vile tukio la kujadili mambo ya Bungeni na taratibu za Bungeni kuonesha kutoridhishwa kwa mwenendo wa Bunge kwenye vikao vya chama ni tukio la kulaaniwa na kukataliwa na kila mpenda demokrasia. Habari ambazo zimekuwa zikitiririka kwa muda wa masaa kadhaa yaliyopita zinatuthibitishia kuwa waoga wanaongoza CCM sasa hivi. Habari za kuwa Spika wa Bunge la Muungano alipewa kibano katika mojawapo ya vikao vya juu vya CCM ni habari za kuudhi, kukera, na kuchekesha; yote kwa kwa wakati mmoja. Vile vile tukio la kujadili mambo ya Bungeni na taratibu za Bungeni kuonesha kutoridhishwa kwa mwenendo wa Bunge kwenye vikao vya chama ni tukio la kulaaniwa na kukataliwa na kila mpenda demokrasia.

Kwa vile CCM wamelewa ugimbi wa madaraka inaonekana hawajui kuwa Bunge siyo tawi la CCM wala Jumuiya ya chama. Spika wa Jamhuri ya Muungano siyo Spika wa Bunge la CCM. Bunge la namna hiyo halipo.

Bunge linaendeshwa kwa taratibu zake na wakati wowote mbunge yoyote hafurahishwi au kuridhishwa na mwenendo wa Bunge taratibu zipo za kutoa malalamiko yake na kama ni kundi kubwa la wabunge basi wana nafasi ya kujadili na hata kumuondoa Spika kwa taratibu za Kibunge (Impeachment).

Lakini CCM imejinyanyua juu na kujiweka kwenye kiti cha enzi ambapo kitu kinachoitwa Katiba hakiangaliwi tena isipokuwa kadi na sheria zilizotungwa na Bunge lenyewe haziangaliwi tena bali taratibu za chama. Imefika mahali watu wanapewa uchaguzi wa "Chama" au "Taifa".

Mjadala wa viongozi hao wa CCM wakiongozwa na Mwenyekiti wao na "vigogo" wengine wa chama hao kuhusu mwenendo wa Bunge au maamuzi ya "Spika" ni mjadala potofu, usio na msingi na kwa hakika ni wa kiwoga!

Kama kuna kundi la wabunge wa CCM ambao wanaamini kuwa Spika hawatendei haki na wao ndio wako wengi Bungeni kwanini wasilete malalamishi yao ndani ya Bunge na badala yake kutumia mbinu za kiviziaji nje ya Bunge? Kama kuna watu ambao wanaona Spika anawapendelea watu wengine kwanini watu hao wasifuate taratibu za Bunge kutoa malalamiko yao?

Hawawezi. Hawawezi kwa sababu wanajua kabisa kuwa Bunge ni mhimili mwingine wa dola na Spika ni Mkuu wa Mhimili huo. Hawawezi kwa sababu wanajua kabisa hawaungwi mkono ndani ya Bunge; Hawawezi kwa sababu wanajua wakizungumza Bungeni Taifa zima litajua nani kazungumza nini na ana hoja gani! Wanaogopa; wanawaogopa Watanzania! Wanaogopa kujulikana!

Ni waoga.

Alichofanya Spika Sitta ni kile vitani kinaitwa "strategic retreat" yaani kurudi nyuma kimkakati ili kujipanga upya. Kama nilivyoandika wiki iliyopita hii ni vita na siyo mapambano. Unaweza ukapoteza pambano moja au mawili lakini mwisho wa siku utashinda vita.

Wao wametumia vikao vya chama, Sitta anawasubiri tena Bungeni. Bunge haliongozwi na Katiba ya CCM au maoni ya wana CCM peke yake. Hivyo, badala ya kuwapa njia rahisi ya kutokea (kumvua uanachama - kitu ambacho nina uhakika hawawezi pamoja na mikwara yao yote!) Sitta ameamua kuwapa ushindi wa pambano moja.

Ndugu zangu mafisadi wanaweza kushinda kwa sababu nyingi lakini kubwa ni kwa sababu Watanzania tumewaachia hivyo. Kuna watu ambao wanatumia hoja ya kuwa "Sitta naye si safi" hoja hii haina msingi! Uchafu wa mtu haumfanyi ashindwe kuona usafi au kuutetea usafi! Mtu mchafu ambaye hataki kusafishika au kufuata usafi wala kuupigia usafi debe ni mchafu per exellence!

Tanzania haiitaji watu wakamilifu (kwani hawapo duniani); Tanzania haiitaji watu watakatifu (wako mbinguni); Tanzania haiitaji watu wasiokosea (hawapatikani); Tanzania inahitaji watu ambao wanajua mapungufu yao, wamesahihisha makosa yao na wanakubali kusahihishwa. Watu ambao wanatukuza uadilifu na wanautafuta sana. Tanzania inahitaji viongozi ambao wanatambua wito wao kuwa ni mkubwa zaidi kuliko makosa au udhaifu wao, watu ambao wako tayari kusahihissha walikokaribu siyo wanaoendelea kunyosha vidole kuwa "fulani naye si safi"!

Ninaamini kwa moyo wangu wote, hakuna kiongozi wa Tanzania sasa hivi ambaye amesimamia wito huu wakuliinua taifa zaidi kama Spika Sitta. Leo hii anasimama kama ngao peke kati ya mafisadi kuliteka Bunge letu na wananchi kulimiliki. Spika Sitta aidha kwa makusudi au kwa bahati mbaya amelipa Bunge letu kile ambacho kwa miaka mingi tumekuwa tukikilalamikia; meno.

Kuna viongozi watatu wa dola yetu; Rais (Utendaji), Jaji Mkuu (mahakama) na Spika (Utungaji wa Sheria na Usimamizi wa serikali). Mhimili hii mitatu katika nchi ya demokrasia haiwezi kuwa pamoja wakati wote. Urais, Mahakama, na Bunge vikikubaliana kwa kila kitu na wakati wote basi tujue kuwa tunaishi kwenye nchi ya Udikteta! Havipaswi kukubaliana kila kitu na wakati wote; ni lazima vigongane.

Hivyo sasa tunashuhudia kugongana kati ya Urais na Bunge na huko tunakokwenda tutashuhudia kugongana kati ya Urais na Mahakama au Mahakama na Bunge. Hii ni sehemu ya demokrasia.

Ni kwa sababu hiyo tunapoona kikundi cha wahuni wachache (namaanisha neno "wahuni" katika kila maana yake mbaya) kujaribu kuliteka Bunge letu na kulijadili pembeni na kutaka lifanye mambo kwa manufaa ya kikundi cha watu hao wachache kwa jina la "chama" ni lazima tuwapinge.

Tunawapinga kwa sababu siyo kazi yao (ni wabunge Bungeni); tunawapinga kwa sababu Bunge si la kwao (ni Bunge la Watanzania); tunawapinga kwa sababu wamefanya kwa woga (wangetaka kuwa majasiri wangesimama Bungeni mbele ya huyo Spika).

Nawataadharisha CCM, makuwadi wa ufisadi na vikaragosi vyao; Msiliteke Bunge wala kusababisha Bunge lisimame peke yake au Spika afanye mambo yamewahi kutokea sehemu nyingine ambako kumekuwepo na mvutano kati ya Bunge na Urais. Ninawahakikishia kuwa mkiendelea kulishambulia Bunge letu namna hii (kama walivyofanya wengine mwaka jana) tutawapinga kwa nguvu zaidi kwani sasa hivi ni Bunge tu linasimama kati yetu na mafisadi waliiokubuhu wanaoshirikiana na mafisadi wa kizungu (wanaitwa wawekezaji) kutugeuza vijakazi wa milele.

Kama mnafikiri mambo hayaendi vizuri, na mnafikiri mna hoja, Bunge lina watu wenu wengi, na Rais anatoka chama chenu; vunjeni Bunge mrudi kwa wananchi sasa! Kama Bunge halichezi ngoma mnayoipiga au kuitikia mlio wa sauti zetu, rudini kwa wananchi mtafute madaraka upya.

CCM mmeruhusu utajiri wetu utweke nyara na mafisadi na sasa mnataka kuteka na Bunge letu? Nyinyi mmechagua CCM ishikeni na ikumbatieni; nyinyi mmechagua kadi za chama chenu zibebeni na mlale nazo; tuachieni Taifa letu; iacheni Katiba yetu!

Mshindwe!

niandikie: This e-mail address is being protected from spam bots, you need JavaScript enabled to view it

Makala hii inaweza kutumika na gazeti lolote lile bila ya kubadilisha mtunzi.
Comments (7)add comment
tembeleh2: ...
Makala iko makini sana, asante mwanakijiji. Mimi nilitaka kuongeza jambo kidogo, Tatizo kubwa la CCM hawaangalii alama za nyakati, wanafikiri mpaka sasa watanzania ni wale wale wa mwaka 47. Kwa kujaribu kumziba mdomo spika sita wamejiweka kitanzini kwa kuwapa ajenda muhimu sana wapinzani wao katika kampeni za ucjaguzi ujao. Mara nyingi wamekuwa wanajisahau kwa kufanya jambo halafu baadae wanakuja kujutia. Lakini mimi naamini kabisa hii ni namna ambayo mungu amepanga ili wananchi waelewe wanatawaliwa na watu wa namna gani. Kazi kwetu watanzania.
1

August 19, 2009
Votes: +4
Auguustine: ...
Asante sana mzee wa kijiji. kwa kweli Chama cha Mapinduzi ya faida ya kwao na si ya sisi tunaowalipa kwa kodi zetu kinasikitisha kwa kitendo kama hiki. Ni aibu kwa wao kukaa kama chama na kumjadili Sitta kwa gharama zetu,huu ni ujinga wao kwa kung'angania madaraka bila kuangalia tuendako. watanzania tubadilike na tuwawape watu wengine nafasi watutumikie na hususani vijana tuichukue nchi hawa wazee hawana jipya.
2

August 19, 2009
Votes: +1
MPENDA HAKI: ...
WATAKE WASITAKE CCM HAIWEZI KUDUMU MILELE! HUO NI UKWELI WA KIHISTORIA NA WA KIROHO. WATAKE WASITAKE SIKU INAKUJA, WATASAMBARATIKA KAMA CHAMA CHA KIKOMUNISTI URUSI, RUMANIA, N.K. ukiona uovu unaitwa haki, na haki inaitwa uovu, na ufisadi unaitwa maadili, na wanaokemea ufisadi wanaitwa watu hovyo, hiyo ni dalili tosha ya kutoweka kwa kikundi fyongo, haijalishi kinatumia mikiki gani!! wanatia kinyaa watu wanaotetea ufisadi, wanatia kinyaa!!
3

August 20, 2009
Votes: +1
David: ...
Mzee MM kweli makala yako ni nzuri sana. Kinachoniuma zaidi ni kuwa ni watanzania wangapiwanaelewa haya? maan utashangaa kuona ccm bado ina wafuasi wengi sana, huwa najiuliza hivi sisi watanzania vichwani mwetu ni wazima kweli au? Mungu atusaidie
4

August 20, 2009
Votes: +1
mwaki: ...
Kwanza ni vema tuelewe kuwa ili kufikia lengo lazima tuwe na mikakati, unajua Mh: David uwezo wa kuwatoa CCM uko mikononi na kichwani mwako wewe na mimi na wengine wanaotaka mambo haya yafanike. ni vema basi tuwe na mkakati wa kuleta mabadiliko. tusaidiane kutafakari yafuatayo.

1)Umekuwa ukipata taarifa hizi za fikra mbadala je ni wangapi wamezipata kupitia wewe?
kumbe unatakiwa usambaze walau kwa watu wote walio kwenye email adress book yako
2)Je unachukua nafasi walau kuwaelimisha watu walio karibuyako masuala ya uraia kama vile umuhimu wa kujiandisha kupiga kura, kwenda kupiga kura na kutafuta habari za wagombeaji.
3) Je umewahi waeleza watu kwanini hatuitaki CCM tena na hivo tulete chama kingine kupitia demokrasia?
kumbe inabidi wewe mwenyewe uelewe kwanza jambo hili kisha waeleze waliokaribu nawe kimantiki sio ushabiki. Mfano makala za mwanakijij ni za kimapinduzi lakini si za kichama hivyo ili kutoleta vurugu na ubishani wafundishe watu kwa pointi zenye mashiko kwa nini CCM hawafai. elezea uchumi wetu, elezea haki zetu,uongozi nk.

Mwishowe kama una uwezo jaribu kusambaza habari hizi kwa wanafunzi wa vyuo vikuu nchini walau kwakufanya hivyo tunaweza leta mabadiliko sio kutamani bila kutenda. Mwanakijiji kwa sehemu anaandiksa makala na habari mbalimbali je si vema kuunga mkono walau kwa usambazaji ili watu wakijua kama wewe watakuwa kama wewe watawaza kama wewe wataona kama wewe.

NAKUPONGEZA KWA MOYO WAKO WA KUPENDA MABADILIKO. UMEIONAJE HIYO??
5

August 20, 2009
Votes: +2
Imbombo nu Bhukifu: ...
Kwanza kabisa nawapongeza timu yote ya Mwanakijiji kwa kazi nzuri ya kutoa taarifa mbalimbali za kuweza kunusuru nchi na watanzania kwa ujumla.

Inaeleweka na kufahamika kuwa hapa Tanzania ukitaka kufanya jambo lolote lazima uwe JASIRI, ujasiri huu wapo wanaoutumia vizuri na wengine wanautumia vibaya. Timu ya Mwanakijiji mko juu, mnautumia vizuri sana. na wale wanachama wenzangu ndani ya chama ambao ni waoga na mashabiki wa ufisadi wanautumia vibaya kupita maelezo.

Mabadiliko ni lazima kwa kitu chochote, ila kinachonisikitisha ni watanzania wengi hawapati elimu ya URAIA, na ndio maana hawajui hata namna ya kuwawajibisha wale wanao waweka madarakani kwa kuwapigia kura. Kwa upande mwingine hata SERIKALI nadhani inafamu hivyo kuwa wananchi wakipata elimu ya URAIA itakuwa tabu kwa viongozi wengi wasio waadilifu. Kama uwezekano wa kutoa elimu kwa mlpa kodi, elimu ya UKIMWI, elimu ya kupambana na rushwa, elimu ya utunzaji wa mazingira, ununuaji wa magari ya kifahali kwa viongozi n.k, inashindikana vipi kupata fedha za kutoa elimu ya URAIA??

Waumini wenzangu, tumeona kuwa Nabii hakubaliki nyumbani , Mh. Sita na wengine wapenda maendeleo ya nchi hii, kwakweli wanawindwa na mafisadi na wapambe wao. Tumombe Mwenyezi Mungu awape ulinzi wa Roho Mtakatifu na wala si wa serikali ya Mh. Pinda kama alivyoomba pale Bungeni.

Mungu yupo nanyi nyoote mnaoipenda Tanzania! Amen!
6

August 21, 2009
Votes: +4
Kisoda2: ...
Asante mkuu,
Hawa jama zetu wa CCM wantuona bado tumelala kama enzi za chama kimeshika hatamu,..wamefulia kisemo cha watoto wa mjini.
Sasa huyu Mahanga naye anashabikia wenzake wa kamuliwe/ama watoswe kwa faida ya wevi wachache.Kumfunga mdomo Sitta ni ujinga wa hali ya juu, na woga usokifani.
Ila nasi kama raia tuahitajika kuliona hili na kulikemea kwa nguvu zote, maana ni hela zetu ndio zinawap kiburi ya kukaa vikao chafu kama hivi na kujadili utumbo kama huu.
Sasa wao walifikiri Sitta atakua mjinga kiasi gani akae kimya wakati njaa ya maendeleo ni kali jimboni kwake na hakunahata fisadi mmoja anakumbuka kupunguza japo shilingi yake moja kuwekeza hapa TZ ili angalau ajira ziwepo na kodi ilipwe kwaajili ya kuliongezea taifa fedha za kuleta maendeleo.
Wanaishia kuzikimbizi nje.
CCM someni alama za nyakati,acheni uhayawani wa miaka ileee.
7

August 21, 2009
Votes: +1

Write comment

busy
 
Ni nani anafaa kuingoza Tanzania kama Rais kuanzia 2010-2015?
 

Photo Albums

Just $6.95/Mo
Unlimited Space, Unlimited Transfer, Free Domain
www.bluehost.com

MwanaKijiji.COM LIVE

Window Player   RealAudioPlayer   Itune Player