MwanaKijiji.COM

Monday
May 21st
Text size
  • Increase font size
  • Default font size
  • Decrease font size
Home arrow Sports arrow Michezo arrow Sita kuachwa safari ya Taifa Stars Sudan
Sita kuachwa safari ya Taifa Stars Sudan
(1 vote)
Written by Nipashe   
Thursday, 04 December 2008
Wachezaji sita wataachwa katika msafara wa timu ya soka ya taifa, Taifa Stars wa kwenda Sudan kwa mechi ya marudiano ya mechi ya mtoano ya kuwania kufuzu kwa fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika zinazoshirikisha wachezaji wa ndani (CHAN).

SoccerKatibu Mkuu wa Shirikisho la soka nchini (TFF), Frederick Mwakalebela alisema wachezaji watakaochwa watajulikana Jumatatu ijayo.

Mwakelebela alieleza kuwa Kocha Mkuu wa Stars, Marcio Maximo atawatangaza wachezaji hao baada ya kutathmini majeruhi na kiwango cha wachezaji hao na kutaja kikosi kitakachoondoka Desemba 11.

Alisema maandalizi ya safari hiyo yanakwenda vizuri na hivi sasa kinachosubiriwa ni mchezo huo.

Mwakalebela alisema pia ili kuiweka sawa timu hiyo wamewapatia makocha mikanda ya mechi za Sudan ili kuweza kuisoma vizuri timu hiyo.

Walio katika hatihati ya kwenda Sudani ni pamoja na nahodha Henry Joseh aliyeumia katika mchezo wa kwanza na mshambuliaji Moses Godwin.

Mchezo utafanyika Desemba 13 jijini, Khartoum na unatazamiwa kuchezeshwa na waamuzi kutoka Kenya.

Stars inahitaji sare ya aina yoyote au kutofungwa chini ya bao moja kutokana na kushinda mchezo wa kwanza 3-1, Jumamosi iliyopita.
Comments (1)add comment
Bavuvi: ...
Good luck to our Taifa Stars
1

December 05, 2008
Votes: +0

Write comment

busy
Last Updated ( Friday, 05 December 2008 )
 
Ni nani anafaa kuingoza Tanzania kama Rais kuanzia 2010-2015?
 

Photo Albums

Just $6.95/Mo
Unlimited Space, Unlimited Transfer, Free Domain
www.bluehost.com

MwanaKijiji.COM LIVE

Window Player   RealAudioPlayer   Itune Player