|
Barabara zote kuu kuwa za lami - Kikwete |
|
Written by Radio One
|
|
Tuesday, 13 May 2008 |
Rais Jakaya Kikwete amesema serikali imedhamiria kuzijenga kwa kiwango cha lami barabara zote kuu, za mikoa na zile za vijijini ili kurahisha usafiri na usafishaji wa bidha na kuharakisha maendeleo ya wananchi na taifa kwa ujumla. Amesema hayo mkoani Mwanza kwenye uzinduzi wa barabara ya Geita Buzilrayombo Kyamyorwa iliyojengwa kwa kiwango cha lami na wakati wa uzinduzi wa ujenzi wa barabara ya Usagara- Geita inayoanza kujengwa kwa kiwango cha lami inayotarajiwa kukamilika mwaka 2010.
Amesema katika kipindi cha miaka michache ijayo serikali itakamilisha mpango wa kuinugnaisha Tanzania na nchi jirani za Kenya, Uganda, Rwanda Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kondo kwa mtandao wa barabara za lami mpango unaojumuisha mtandao wa barabara za ukanda wa ziwa Victoria na mtandao barabara za ukanda wa kati na kusini. Mapema Waziri wa Miundombinu Dakta Shukuru Kawambwa alisema azma ya serikali ya kujenga kwa kiwango cha lami barabara ya kutoka Mtwara hadu Mtukula mkoani Kagera iko mbioni kufikiwa, kwani hadi sasa ni kilomita 290 tu zilizosalia katika kilomita 2130, na kwamba hatua hiyo itafikiwa mwaka 2010. Rais Jakaya Kikwete leo anatarajiwa kukamilisha ziara yake ya siku mbili mkoani Mwanza kwa kuzindua kiwanda cha kusindika minofu ya samaki cha TFDC kinachomilikiwa na kampuni ya uwekezaji ya watanzania ya NICOL, kiwanda ambacho mwaka jana alikiwekea jiwe la msingi.
|